Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Kusini Comred Abdallah Makame (wa kwanza kulia) akifafanua jambo leo tarehe 18/7/2023 kwa Kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ialla wakati walipotembelea eneo la kufanya uwekezaji wa pamoja Jumuiya hizo mbili Jimbo la Makunduchi, Wilaya ya Kusini.
…….
NA NOEL RUKANUGA, WILAYA YA KUSINI – ZANZIBAR
Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ialla chini ya Mwenyekiti Comred Mohamed Ramadhani Msofe leo tarehe 18/7/2023 wametembelea eneo ambalo wanatarajia kufanya uwekezaji wa pamoja na Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya Kusini – Zanzibar.
Akizungumza leo tarehe 18/7/2023 Wilaya ya Kusini baada kutembelea eneo hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ilala Comred Msofe, amesema kuwa ushirikiano wa Jumuiya hizo mbili utasaidia kuleta tija katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Kusini Comred Abdallah Makame, amesema kuna maeneo mawili ambayo wanatarajia kufanya uwekezaji wa pamoja ambayo yapo Jimbo la Paje na Makunduchi.
Amesema kuwa uwekezaji huo wa pamoja utasaidia kuimarisha muungano uliopo Tanzania Bara na Zanzibar ambapo kwa saaa bado wanangalia aina ya mradi ambao wanaweza kufanya ili kuleta tija.
“Tumetafuta maeneo hayo ili tuweze kujitegemea kiuchumi, pia kuendeleza undugu na umoja wa kisiasa” amesema Makame.
“Tuendelee kutumisha umoja wetu, wakati umefika kuwa na mshikamano wa pamoja na kuacha mvutano kusemana huyu wa Zanzibar, huyu wa Bara” amesema Makame.