Wananchi wa Kusini Unguja Zanzibar wakisherekea Sherehe za Kogwa (Mila) zilizofanyika leo tarehe 17/7/2023 Makunduchi .
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Bw. Mohamed Msofe akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Chama Cha CCM Wilaya ya Ilala Bi. Amina Fumbwe katika sherehe za kogwa zilizofanyika leo tarehe 17/7/2023 Kusini Unguja Zanzibar.
Wananchi wa Kusini Unguja Zanzibar wakisherekea Sherehe za kogwa (mila) zilizofanyika leo tarehe 17/7/2023 Makunduchi.
Wananchi wa Kusini Unguja Zanzibar wakisherekea Sherehe za kogwa (mila).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kusini Unguja akifafanua jambo katika kikao kazi leo kabla ya Jumuiya ya Wazazi Ialla kwenda kushiriki Sherehe za kogwa
Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ilala wakiwa katika kikao leo tarehe 17/7/2023 Kusini Unguja.
Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala, pia Diwani wa Kata ya Kariakoo, Bw. Abdulkarim Masamaki akizungumzia umuhimu wa ziara katika Chama.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Buguruni Bi. Jamira Kumbilamoto akizungumzia umuhimu wa ziara katika Chama.
NA NOEL RUKANUGA, UNGUJA KUSINI – ZANZIBAR
…………….
Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala leo tarehe 17/7/2023 wameshiriki Sherehe za kogwa ( Utamaduni) zilizofanyika Makunduchi Kusini Unguja Visiwani Zanzibar.
Ushiriki wa Sherehe hizo ni sehemu ya ratiba ya Jumuiya ya Wazazi CCM ilala katika ziara yao ya siku tano Zanzibar ambapo leo ni siku ya pili tangu wawasili kusini unguja.
Akizungumzia Sherehe hizo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCm Wilaya ya Ialla Mhe. Mohamed Msofe, amesema kuwa wamejifunza mambo mengi ambayo wamekuwa wakifanya Jumuiya ya Wazazi Kusini Unguja.
“Wazazi CCM Ialla na kusini Unguja tumeingia makubaliano ya ushirikiano wa kazi katika sherehe za utamaduni tumejifunza na tumefurai kwa ukalimu wao” amesema Mhe. Msofe.
Mhe. Msofe amesema kuwa lengo kuimarisha Jumuiya ya wazazi, kujifunza mambo mbalimbali ya kikazi yanayofanyika kusini unguja.
Amefafanua kuwa katika ziara hiyo ya siku tano watafanya mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo kufanya usafi, kutembelea wagonjwa, kusafisha mazingira, kupanda miti, kutembelea Shule.
“Tutakutana wazee wa Chama Cha CCM kusini unguja ili kuchota busara zao pamoja na kupata historia ya chama” amesema Bw. Msofe.
Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala, pia Diwani wa Kata ya Kariakoo, Bw. Abdulkarim Masamaki, amesema kuwa ziara hiyo ni muhimu kwa Jumuiya katika kuhakikisha wanaendelea na ushirikiano wa CCM kusini Unguja.
“Tumepata makaribisho mazuri kutoka kwa wenyeji wetu kupitia ziara hii inakwenda kuleta mafanikio manufaa katika Jumuiya yetu na kupiga hatua” amesema Bw. Masamaki.
Hata hivyo wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Ilala walioshiriki ziara hiyo wamefuraishwa na ushirikiano uliopo baina ya Jumuiya hizo mbili, huku wakieleza unakwenda kuleta maendeleo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Buguruni Bi. Jamira Kumbilamoto, amesema “Tutegemee mazuri kupitia ziara hii katika kuleta na mafanikio ndani ya Jumuiya, kwani wezentu wametupa eneo ambalo tunaweza kujenga kujenga hotel kama sehemu ya mradi” amesema Bi Kumbilamoto.
Naye Bi. Bahati Mohamed, amesema kuwa wanaendelea kujifunza masula ya kiuchumi, siasa kutoka kwa wenyeji wetu kutokana mambo mbalimbali waliofanya katika Jumuiya Kusini Unguja.