BENKI ya Standard Chartered Tanzania imesisitiza dhamira yake ya kuendeleza mbele gurudumu la maendeleo ya wananchi kiuchumi nchini.
Hivi karibuni Benki hiyo,ilifikia makubaliano na Benki ya Access Plc kuhusiana na huduma za kibenki kwa wateja, binafsi na biashara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Benki hiyo leo Jijini Dar es Salaam imesema kuwa Benki ya Access itasimamia huduma za kibenki kwenye nchi zilizotajwa hapo juu.
Taarifa hiyo ilisema kuwa huduma zilizotajwa hapo juu zitabaki zitategemea kutoka kwa mdhibiti wa Benki hiyo nchini Nigeria.
Access Bank ina mtandao wa zaidi ya matawi 600 katika mabara matatu,masoko 18 na wateja wanaofikia milioni 52.
Benki ya Standard Chartered na Access Bank Plc (Access) zilifikia makubaliano ya kuuza hisa za Standard Chartered katika kampuni zake tanzu za nchini Angola, Cameroon,Gambia na
Sierra Leone, pamoja na Biashara yake ya wateja,Binafsi na Biashara ya Benki nchini Tanzania ,kwa kutegemea idhini ya udhibiti.
Benki ya Access itasimamia shughuli zote katika nchi zilizotajwa, na kuhakikisha uendelevu kwa wafanyakazi na wateja. Mpito huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12 ijayo.
Taatifa hiyo imebainisha wazi kuwa nchini Tanzania, haitajiondoa kutoa huduma za Biashara kwa wateja,Binafsi na biashara ya Benki maarufu kama rejareja ili ku shughukika za kibenki kwa mashirika na Taasisi.
Access Benki itatoa huduma mbalimbali za kibenki na uendelevu wanhuduma kwa wateja wake ikiwemo waajiriwa na wateja wa iliyokuwa Standard Chartered Benki katika nchi tano zikizotajwa hapo juu.
Benki ya Access Bank na Standard Chartered ziitafanya kazi kwa karibu katika kipindi cha mpito cha miezi 12 ijayo. work closely together in the
Akizungumzia makubaliano yalifikiwa Mtendaji mkuu wa Benki ya Standard Charter Tanzania, Herman Kasekende,alisema kuwa Benki hiyo imekuwepo chini kwa zaidi ya miaka 106 na ina amini katika mipango ya nchi ya muda mfupi na mrefu..
Kasekende aliwahakikishia wateja wa benki hiyo kuwa huduma zote na mtandao wa benki zitaendelea kutolewa kwa makubaliano na Acceas Benki.
“Tunaamini tumefikia mafanikio makubwa zaidi kwa kuwafanya wateja wetu watuamini kama ni sehemu pekee ya wao kuwekeza,” alisema mtendaji mkuu huyo.
“Wakati mipango ijayo ya benki ,tumefarijika na ukuaji na ustawi wa benki yetu katika Bara la Afrika na dhamira ya Benki inabaki ileile ya kuwahudumia watanzania,” aliongeza.