Adeladius Makwega–MWANZA
Wakristo wameambia kuwa ya jumapili ya 15 ya Mwaka A wa Liturjia ya Kanisa, wanaalikwa kulisikia neno la Mungu , wanaalikwa kulipokea neno la Mungu, linalopandwa kama mbegu katika mioyo yote na kulisikia neno hilo lipate kuzaaa matunda mema, moja mia, moja sitini na moja thelathini.
Hayo yamesemwa na Padri Samsoni Masaja katika misa ya jumapili ya Julai 16, 2023 katika Kanisa la Bikira Maria Imekulata na Paroko wa Parokia ya Malya , Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.
“Sisi tuliochagua kuwa watoto wa Mungu, zaidi ya kulidhihirisha hilo, kwa kukubali kubatizwa, hapo tunapewa utume usiorudi nyuma, utume unaosonga mbele, utume huo Kristo ameweka bayana pale anapowaagiza mitume wake, anawaambia wakahubiri injili kwa kila kiumbe, kwa watakaokubali kuwabatiza kwa jina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu.
Huo ni utume wetu sisi tulio tayari kudhihirisha kuwa sisi ni wana wa Mungu na sisi wana wa Kanisa. Utume huo ni wa kulibeba neno la Mungu, kumtangaza Mungu, azidi kujulikana Ulimwenguni, ili utume huo uzae matunda mema kwa wengine pia uzae matunda mema kwetu wenyewe n ahata sisi tunaohubiri hili tuonekane katika matendo yetu .”
Akiendelea kuhubiri katika misa ya kwanza inayoanza saa 12 kamili ya asubuhi kila ya jumapili Padri Masanja alisema kuwa mfano wa mpanzi una makundi haya; mfano wa mbegu iliyopandwa njiani, iliyopandwa katika mwamba, iliyopandwa katika miba na ile iliyopandwa katika udogo mzuri, aliuliza je mimi na wewe ni mbegu iliyopandwa wapi?
Aliendelea kuhubiri huku akirejea somo la Nabii Isaya kuwa kile kinachosemwa lazima kiwe kinatendwa na sote na hata yule asemaye.
Misa hii iliyofanyika katika hali ya utulivu mkubwa, labda tu juu ya paa la Kanisa hilo zikisikika tu sauti ya dege wa Korongo(Cranes) waliopo katika familia ya ndege ya Gruidae ambao ni ndege maarufu sana katika viunga vya Malya, ambapo wenyeji wa Malya wanasema ni ndege wanaokula nyoka .
Misa iliendelea vizuri huku ikiwa na nia na maombi kadhaa, mojawapo ya maombi hayo lilikuwa hili,
“Ulimtaja shetani kama hatari kubwa, utuamshe tukeshe, tusije tukashindwa kwa hila za shetani”
Wakati wa matangazo ya Misa hiyo Padri Samsoni Masanja alimualika muumini Amanus Kezinjo ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa Jumuiya mojawapo katika Parokia hiyo, akiwa pia askari wa Jeshi la Magereza Tanzania alisimama mbele ya marufaa ya kanisa hilo na kuwaaga waamini wenzeka baada ya kuhamishwa kituo cha kazi.
Padri Msanja alitambulisha Frateli Francis Makungu Igosha akitokea Seminari ya Mtakatifu Paulo Kipalapala huku akiwa mzaliwa wa Parokio Ibingili Magu Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.ambaye atakuwepo Parokia hapo kipindi cha likizo yake.
Kwa hakika hadi misa hiyo ya kwanza inamalizika, hali ya hewa ya Malya na viunga vyake ilikuwa ni ya baridi nyakati za asubuhi, jua kali wakati wa mchana, huku majani yakiendelea kukauka lakini mifugo bado inachungwa umbali mfupi na makazi wa wakazi wa Malya , wilayni Kwimba-mkoani Mwanza.