Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan awezesha rasilimali katika mapambano dhidi ya UKIMWI
Kauli hiyo imebainishwa na Waziri wa Afya Mhe, Ummy Mwalimu wakati akielezea mpango wa kutokomeza UKIMWI ifikapo 2030 huku akielezea kua mafanikio ya kudhibiti UKIMWI nchini yameongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha rasilimali katika mapambano ya virusi hivyo.
Aidha Waziri Ummy amesema UKIMWI utatokomea ifikapo mwaka 2030 ambapo hadi sasa 96% ya Watanzania wanaoishi na VVU wanajua kuwa wana maambukizi, 98% ya wanaoishi na VVU wanatumia dawa ARVs, 97% ya wanaotumia dawa wamefubaza makali ya UKIMWI.
Hata hivyo, Waziri Ummy amesema Tanzania imejipanga kuutokomeza UKIMWI kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO kwa kuanzisha sera ya kupima na kutoa dawa kwa waathirika wa virusi hivyo.
“Tanzania pia imekuwa ikizingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na WHO/UNAIDS ili kutokomeza UKIMWI ikiwemo kuanzisha Sera ya kupima na kutoa dawa (Test and Treat) kwa Watu wanaobainika kuwa VVU bila kusubiri kigezo cha idadi ya CD4, utoaji dawa za kuzuia maambukizi ya VVU kwa makundi yenye hatari zaidi ya kuambukizwa VVU”, amesema.
Aidha Waziri Ummy, amebainisha njia ambazo zitasaidia katika mapambano hayo ya kuutokomeza UKIMWI ifikapo 2030 ikiwa ni pamoja na Kuimarika kwa Ufanisi wa huduma za VVU kama vile uibuaji wa watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI na Utoaji dawa za kuzuia maambukizi ya VVU kwa makundi yenye hatari zaidi ya kuambukizwa VVU.
Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa, njia nyingine ya kutokomeza UKIMWI ni pamoja na kufata uongezaji wa ufanisi katika uibuaji wa watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI na utoaji wa Kondomu hadi kwenye ngazi ya jamii
Hata hivyo Wazir Ummy amesema Kurahisisha Utoaji wa ARV kwa kuanza afua ya kutoa dawa za muda wa miezi mitatu hadi sita na Kuwepo na nafasi mpokea huduma kuchagua sehemu na muda atakaokuja kupokea huduma ni miongoni mwa njia ambazo zitatokomeza UKIMWI nchini ifikapo 202