…………………..
Na. Sixmund J. Begashe
Wananchi waishio jirani na Hifadhi ya Taifa Mikumi wameanza kunufaika na Utalii wa Utamaduni baada ya Mradi wa Kukuza na Kuendeleza Utalii Kusini mwa Tanzania, kuviwezesha vikundi mbalimbali ili viweze kunufukaika na ujui mkubwa wa Watalii katika Hifadhi ya Taifa Mikumi unaotokana na Matokeo chanya ya Filamu ya The Royal Tour.
Msimamizi Mkuu wa Mradi wa (REGROW) Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aenea Saanya amesema kuwa, Vikundi zaidi ya 15 Vikiwemo Cha Bega Kwa Bega Kokoba Group na Masai Bomba, Mkoani Morogoro, Vimenufaika na Mradi huo, kielimu na biashara ya mazao ya Utamaduni na nyinginezo ili kuiambatanisha jamii zinazoishi jirani na Hifadhi na Utalii pamoja na Uhifadhi endelevu.
Akizungumzia namna walivyonufaika na Mradi wa REGROW, Mwenyekiti wa Kikundi Cha Masai Boma, Nuhu Ole meleni, amefafanua kuwa, baada ya Kuwezeshwa na Mradi huo, wanakikundi wameweza kuanzisha Biashara ya Kazi za Sanaa zenye asili ya Kimasai na kupata fedha zinazo wawezesha kusomesha watoto wao pamoja na Mambo mengine mengi ya kifamilia.
Bw. Meleni, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuona umuhimu wa Mradi huo uwanufaishe jamii moja kwa moja huku ukishugulika na Maboresho Makubwa ya Miundombinu pamoja na Kutangaza vivutio vya Utalii Kusini mwa Tanzania hivyo kwa sasa wanapata kwani wanapata watalii wengi wanaofika na kununua bidhaa zao za Kiutamaduni.