Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akihimiza ukamilishaji mradi wa ujenzi wa miundombinu elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya TEMEKE wakati wa ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utelezaji wa miradi ya SEQUIP na BOOST.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akielekea kukagua miundombinu ya elimu katika shule ya Msingi Mkodongwa inayojengwa kupitia mradi wa BOOST katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akisikiliza hoja ya Mbunge wa Temeke Mhe. Abdallah Chaurembo, wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo ya kukagua ujenzi wa madarasa katika Shule ya Sekondari ya Imani inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi kuzungumza na wananchi wa Tundwi Songani na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, wakati wa ziara ya Mhe. Ndejembi ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Tundwi Songani inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP
…………………….
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi wa Tundwi Songani na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa shule hiyo inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP.
…………………..
Na: James Mwanamyoto (OR-TAMISEMI)
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka wanafunzi wa shule mpya za sekondari zilizojengwa kupitia mradi wa SEQUIP kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili kupata ufaulu mzuri katika mtihani wa kidato cha nne.
Mhe. Ndejembi ametoa wito huo kwa wanafunzi, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu inayojengwa kupitia mradi wa BOOST na SEQUIP katika Halmashauri za Manispaa ya Temeke na Kigamboni.
Mhe. Ndejembi amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya elimu nchini ili kuwawezesha wanafunzi kupata ufaulu mzuri.
“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa fedha nyingi kuboresha miundombinu ya elimu kwa lengo la kuwapatia wanafunzi elimu bora kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Kuhusiana na changamoto zinazokwamisha ujenzi wa miundombinu ya elimu nchini, Mhe. Ndejembi amesema Serikali itahakikisha inazitafutia ufumbuzi changamoto hizo ndani ya kipindi kifupi ili miundominu hiyo ikamilike kwa wakati na kuanza kutumika.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Halima Bulembo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya wilayani kwake katika eneo la Tundwi Songani ambalo liko pembezoni na linakabiliwa na changamoto nyingi zikiwepo za miundombinu ya barabara na afya.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha kupitia mradi wa SEQUIP ili kujenga shule mpya ya kimkakati ndani ya jimbo lake.