………………….
Na Sixmund J. Begashe
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi ya Wanyamapori Pasiansi imepongezwa kwa Mafunzo na program mbalimbali inazoendesha kwa lengo la Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria.
Wakipita kwenye Banda la Maliasili na Utalii lililopo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Saba Saba) Jijini Dar es Salaam, wananchi wengi wamevutiwa na uwepo wa Chuo hicho ambacho kinatoa mchango mkubwa nchini katika Uhifadhi na ulinzi wa Raslimali za Taifa.
Bw. Chance Enock ambaye ni Mkazi wa Chalinze, amesema, Mafunzo yanayotolewa na Chuo hicho, yanaendelea kuwa muhimili katika ulinzi wa Wanyamapori, katika maeneo yaliohifadhiwa kisheria pamoja na wananchi wanaoishi pembezoni mwa Hifadhi za Taifa.
“Mwenyezi Mungu katujalia raslimali lukuki, kama si mikakati ya Serikali yetu ya kuwa na Chuo hiki na vinginevyo kunoa vijana wakuilinda, sisi tusinge nufaika nayo na tungekosa kitu cha kurithisha watoto wetu, kwa kweli nimeelimika na ujio wangu hapa 77 ,”. Alisema Bw. Enock
Akizungumzia chuo hicho kilichopo Mkoani Mwanza, Makamu Mkuu wa Chuo Mafunzo, Utafiti na Ushauri elekezi, Bi. Ester Mtamenywa- amesema Chuo kinatoa ujuzi wa kozi za Usimamizi wa Wanyamapori na Hima Sheria, Kuongoza Wageni , na Usalama wa Wageni. Pia Chuo kinaendesha Kampuni ya Ulinzi – Pasiansi Security Company( PASCO)ambayo inatoa huduma kwenye maeneo yaliyo hifadhiwa, ametoa wito Kwa wananchi na wadau mbalimbali kushirikiana na chuo hicho kwa maslahi mapana ya nchi.