Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka Watanzania kutembela Makumbusho na malikale nchini ili kujua historia ya nchi yao.
Mhe. Masanja ameyasema hayo alipotembelea Banda la Maliasili na Utalii katika Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba).
Amesema Tanzania kuna vivutio vingi ikiwemo vituo vya Makumbusho na Malikale ambavyo vinaelezea mambo mbalimbali ikiwemo historia adhimu ya nchi ya Tanzania
“Ukitembelea katika vivutio hivi unajifunza historia ya nchi, unapunguza msongo wa mawazo na kuongeza pato la Taifa” amesema Mhe. Masanja.
Amesema Serikali inatia mkazo juu ya uendelezaji wa makumbusho na malikale na kwamba wananchi sasa wanaruhusiwa kuanzisha makumbusho binafsi.
Mhe Masanja amesema uanzishwaji wa makumbusho binafsi utachochea utalii na kupanua wigo wa utalii kwa watalii wa ndani na nje ya Tanzania wanaotembelea maenwo hayo.