Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amepokea nakala za hati za
utambulisho za Balozi Mteule wa Pakistan hapa nchini, Mhe. Siraj Ahmad Khan
katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 12 Julai 2023 katika Ofisi Ndogo za Wizara
jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao,
Mhe. Dkt. Tax amemkaribisha nchini Mhe. Khan na kumuahidi ushirikiano kutoka
kwake binafsi, Wizara na Serikali kwa ujumla wakati wote atakaokuwa nchini
akiiwakilisha nchi yake.
Aidha, amesema kuwa, ushirikiano
kati ya Pakistan na Tanzania ni mzuri na utaendelea kuimarika kupitia Balozi
Khan kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.
Naye Mhe. Khan ameeleza
furaha yake kuwa Tanzania na kwamba yupo tayari kutekeleza majukumu yake ya
uwakilishi kwa kushirikiana na Wizara na Serikali kwa ujumla kwa maslahi mapana
ya nchi hizi mbili.
Mhe. Dkt. Tax akimsikiliza Mhe. Khan wakati wa mazungumzo yao. |