Mkuu wa wilaya ya Same Kasilda Mgeni ametoa mwezi mmoja kwa viongozi wa Vijiji vitatu vya Tae, Mahande na Heikondi vilivyo kata ya Tae wilayani humo kushirikiana na wakazi wa humo kuteketeza mashamba yote ya Mirungi na kuachana na zao hilo haramu.
Ameagiza viongozi wa Halmashauri kusimamia zoezi hilo na kutumia wataalam wa Idara ya Kilimo kufanya utafiti na kuainisha mazao mbadala yanayostawi katika eneo hilo, na kutoa elimu kwa wananchi waweze kunufaika.
Ameyasemahayo katika mkutano wa hadhara maalum kueleza zoezi linaloendelea kuteketeza Mashamba ya Mirungi linaloongozwa na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya wakishirikiana na vyombo vingine vya Usalama.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya DCEA.Aretas Lyimo amesema Oparesheni hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani ambapo wamefanikiwa kuteketeza Ekari 535 katika vijiji hivyo vitatu ndani ya siku saba.