Na John Walter-Mbulu
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James, amewataka wakulima wilayani humo kuweka akiba ya chakula Cha kutosha ajili ya matumizi ya familia ili kuepuka changamoto ya njaa inayoweza kutokea kutokana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi.
Ameyaeleza hayo akiwa katika ziara ya kikazi katika Kata ya Bargish, Daudi na Marang ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake katika kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
Aidha amewahimiza na wafugaji kuhakikisha katika pesa wanayo pata katika mauzo ya mifugo yao, watumie kiasi cha fedha hizo kununua chakula na kuweka akiba.
Pamoja na mambo mengine Komred Kheri James ameitumia ziara hiyo kukagua miradi ya maendeleo, kuhamasisha shughuli za maendeleo na kusikiliza kero za Wananchi.
Kwa upande wa utekelezaji wa miradi Komred Kheri James ameipongeza Halmashauri ya Mji wa Mbulu kwa usimamizi wa miradi ya Elimu, na ameelekeza Halmashauri iwekeze nguvu za kutosha kukamilishwa miradi ilio anzishwa na wananchi ili iweze kukamilika na kutumika.