Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi akifafanua jambo. PICHA| MPIGAPICHA WETU
…………………..
Shabiki wa timu ya Yanga na Manchester United Ezekiel Mwang’onda (34) amesema ndoto yake ya miaka saba katika kubashiri imekuwa kweli baada ya kushinda kitita cha Shilingi Milioni 234,272,830 kupitia mchezo wa Perfect12 wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania.
Mwang’onda ambaye ni mjasiriamali ameshinda mamilioni baada ya kubashiri kwa usahihi jumla ya mechi 12 za ligi mbalimbali duniani.Alisema kuwa amekuwa akibashiri kwa kipindi kirefu bila mafanikio, lakini mara baada ya kujishughulisha na kampuni ya M-Bet, amepata bahati kwa muda mfupi sana.
“Nimekuwa nikibashiri kwa takribani miaka saba sasa, hivi karibuni, nikaamua kubashiri na M-Bet kwa sababu kubwa tatu, sababu ya kwanza ni dau, ambapo unatumia sh1,000 tu kubashiri mechi 12, sababu ya pili idadi ya washindi ambao wamekuwa wakishinda mara kwa mara na tatu, uharaka wa kupata fedha za ushindi na huduma bora kwa washindi.Sababu hizi tatu zimenifanya kuhamia huku na sasa nimeingia nyumba ya mabingwa ambao pia ni mamilionea,” alisema
Mwang’onda.Alisema kuwa pamoja na shughuli nyingi kusimama, M-Bet iliendelea kuweka mikeka ya kubashiri ikishirikisha mechi mbalimbali pamoja nanchi za Amerika ya Kusini.“Mimi mara nyingi huwa sifuatilii ligi za Amerika ya Kusini, hata hivyo sikuacha kubashiri na kuendelea kufuatilia kuweka dau na M-Bet na kushinda kiasi kikubwa cha fedha.
Nina majukumu kibao, fedha hizi nilizoshinda, zitasaidia kukuza biashara yangu na kuwekeza katika miradi mingine,” alisema Mwang’onda ambaye ni mkazi wa Kyela, mkoani Mbeya.Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema Mwang’onda ameungana na washindi wengine wa droo ya Perfect12 na kuwaomba Watanzania wenye umri zaidi ya miaka 18 kuendelea kubashiri kupitia michezo yao mbalimbali ili kushinda fedha na kubadili maisha.
“Nampongeza Mwang’onda kwa ushindi huu mkubwa na kikubwa zaidi. Nawaomba vijana wenye umri kuanzia miaka 18 kubashiri na M-Bet ili kujaribu bahati yao,” alisema Mushi.