Katika kutoa Huduma za makazi bora kwa watumishi wa umma Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) inatoa punguzo kwa wapangaji wa nyumba zake kwa kutoza asilimia 77 ya Bei ya soko au kutoa punguzo asili 33 ya Bei ya soko.
Kama Nyumba inapangishwa shilingi Mil. 1 mtumishi atalipa shilingi laki saba na elfu Sitini na Nyingine serikali itamalizia.
Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja Mawasiliano na Masoko Bw. Fredrick Kalinga wakati akielezea mikakati ya TBA alipokuwa akizungumza katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Leo Julai 10,2023.
Kalinga ameeleza kuwa Kwa Upande wa mwananchi wa kawaida ataruhusiwa kupangisha lakini asilimia 33 haitokuwepo Kwa sababu ni Nyumba ambazo zimejengwa kwa kutumia Fedha za ndani.
Ameeleza kuwa kuna matumaini mapya kwa watu wasiokuwa watumishi wa Umma kwani Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa maagizo kuwa Sheria iliyoanzisha Wakala wa Majengo Tanzania TBA irekebishwe na Ili shirika liweze kupata nafasi ya kushirikiana na sekta binafsi baada ya kupokea maelekezo hayo wameweza kuyafanyia Kazi na wamefikia hatua nzuri.
Pia Kalinga ameongeza kuwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ipo hatua za mwisho za kukamilisha maboresho hayo ya sheria ili kushirikisha sekta binafsi katika baadhi ya miradi kwa maendeleo ya taifa