Wakala wa Majengo nchini TBA wameendelea kufanya ubunifu kwenye majengo mbalimbali ya serikali ili ikamilike kwa wakati ambapo wameweza kupata maoni na kutoa elimu kwa watembeleaji wa maonesho jinsi ya kusimamia miradi hiyo.
Hayo yameelezwa Leo kwenye Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika Kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Meneja Mawasiliano na Masoko (TBA) Fredrick Kalinga
Amesema ubunifu walioufanya kwenye Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma imepelekea kupata watu wengi waliojitikeza kujua ubunifu huo na ukubwa wa ekari zilizotumika.
“Ujenzi wa ikulu ya DODOMA ambayo umejengwa na Suma JKT sisi TBA Tukiwa washauri elekezi katika mradi umevutia watu Wengi sana kujifunza kuhusu ubunifu tuliofanya”amesema Kalinga
Amesema TBA wamefanya ubunifu pia kwenye mji wa serikali Mtumba DODOMA kwa kujenga majengo ya wizara 17 kati ya wizara 27 yanayojengwa pamoja na majengo ya taasisi.
Ameongeza kuwa mpaka Sasa wanatekeleza ujenzi wa jengo la ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kama wakandarasi pamoja na kwamba miradi mingine wanashiriki kama washauri elekezi.
Amesema pamoja na ujenzi wa mji mkuu wa kiserikali DODOMA lakini pia wanatarajia kufanya marekebisho ya viwanja vya michezo kama uwanja wa Taifa na vingine.
Sambamba na hayo Kalinga amesema wameendelea kufanya kazi zao huku wakitoa Rai Kwa wananchi kutembela kwenye banda lao ili wapate elimu kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na TBA
Amesema TBA bado inaendelea na ujenzi wa nyumba tofauti ambapo kutakua na nyumba za chini,Vila na bangaloo lakini nyumba za Ibada,viwanja vya Mpira shule n.k. katika mradi wa Ujenzi wa nyumba 3500 katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma
Kalinga amesema kuwa baadhi ya maeneo mengine ambayo wanafanya Ujenzi ni pamoja na Dar es salaam ambapo wanaendeleza Ujenzi wa jengo la Gorofa 6 eneo la Masaki , Canadian ambalo litakuwa na jumla ya familia 12.
“Katika Mwaka huu wa Fedha pia tunategemea
kuwa na Ujenzi wa Gorofa katika Mkoa wa Arusha eneo la Arusha Mjini ambalo litakuwa na Gorofa sita”amesema Kalinga