Afisa Sheria Mwandamizi, Kurugenzi ya Huduma Sekta ya Kifedha, Bw. Ramadhani Myonga akizungumza kuhusu namna taasisi za fedha zinatakiwa kutoa elimu ya fedha kwa wateja wao ili kujenga uelewa wa kiuchumikwa wananchi.
Baadhi ya wananchi waliotembelea katika banda la BoT wakifurahia jambo na Maafisa wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Huduma za Kurugenzi ya Ujumuishi na Ustawi wa Huduma za Fedha, Bw. Lucas Maganzi katikati na Afisa Sheria Mwandamizi, Kurugenzi ya Huduma Sekta ya Kifedha, Bw. Ramadhani Myonga wakati walipokuwa wakipata eimu ya fedha katika banda hilo.
…………………………………………
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezitaka Taasisi za Fedha nchini kuwa na utamaduni wa kutoa elimu kwa wateja wao hasa wanaohitaji huduma ya mkopo ili kuleta tija na Kila mmoja kunufaika na mikopo hiyo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam , Afisa Sheria Mwandamizi, Kurugenzi ya Huduma Sekta ya Kifedha, Bw. Ramadhani Myonga, amesema kuwa fedha inahitaji nidhamu ili uweze kufanikiwa na kupiga hatua katika shughuli yoyote unayofanya ya maendeleo.
Amesema kuwa wamekuja katika maonesho ya Sabasaba kueandelea kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda la BoT kuwafundisha na kuwaelimisha namna ya kutengeneza bajeti pamoja na Kuweka kipaumbele, Kuwekeza pamoja na Kulipa kodi.
Amesema kuwa pia wanatoa elimu ya namna bora ya kupangilia matumizi kulingana na mapato ili kutengeneza mazingira rafiki katika uchumi.
“Pia tunatoa elimu ya kuweka akiba na kutoa ufafanuzi wa akiba kwa kuweka katika taasisi za fedha, vyama vya ushirika na sehemu nyengine rasmi” Amesema Bw. Myonga
Amefafanua kuwa pia wanaendelea kutoa elimu ya fedha kwa ajili ya watoto kwani ni muhimu kujifunza kwa kutengeneza msingi mzuri wa kuweka akiba wakiwa na umri mdogo ili kuwajenga namna ya kusimamia shghuliza kuichumi wakiwa bado wadogo.
“Katika maonesha ya mwaka huu pia tumekuja na elimu kwa ajili ya wananchi na taasisi za fedha kwa ajili ya kuangalia namna nzuri ya kutoa mikopo ili kila mmoja kwa nafasi yake aweze kunufaika na mikopo hiyo”