Meneja wa huduma ndogo za fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Robert Mshiu akizungumza kuhusu huduma ndogo za fedha na utekelezaji wa sheria kwa wadau katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijiniDar es Salaam.
Meneja wa huduma ndogo za fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Robert Mshiu akizungumza kuhusu huduma ndogo za fedha na utekelezaji wa sheria kwa wadau katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijiniDar es Salaam.
Wananchi mbalimbali wakipata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na Benki Kuu ya Tanzania BoT zikiwemo huduma ndogo za fedha.
…………………………………..
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema watawachukulia hatua za kisheria taasisi ndogo zinazotoa huduma za fedha ambazo zinakwenda kinyume na taratibu za sheria na kanuni zilizowekwa katika Leseni.
Akizungumza leo tarehe 7/7/2023 Jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, Meneja wa huduma ndogo za fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Robert Mshiu, amesema kuwa zipo taarifa kuna taasisi ambazo zimepata leseni lakini hazitekelezi matakwa ya sheria.
“Tunaendelea kuwafuatilia kwa ukaribu ili kuhakikisha tunawachukuliwa hatua kali za sheria watu wote ambao hawafuati taratibu” amesema Bw. Mshiu
Amesema kuwa kutofuata sheria ni pamoja na kufanya biashara ya fedha bila kuwa na leseni kwani ni kosa la jinai.
“Wananchi kabla ya kutumia huduma ndogo za fedha katika taasisi yoyote wanapaswa kupata taarifa sahihi kwa hiyo taasisi, pia waingie mkataba na kuielewa vizuri ikiwemo kiasi cha riba wanachopaswa kulipa ili wakubaliane na masharti” amesema
Amefafanua kuwa sheria hizo zimegawanywa katika madaraja manne ambazo ni taasisi ndogo za fedha zinazopewa dhamana, makampuni, vyama vya ushirika vya kuweka akiba na kukopa pamoja na vikoba.
Amesema kuwa sheria hiyo imeanza kutekeleza ikiwemo na lengo ya kuitaka sekta ndogo ya fedha kuwa rasmi na kuzifanya kuwa taasisi za fedha kama zilivyo taasisi nyengine zikiwa zimesajiliwa na kupewa Leseni kutoka BoT.
Bw. Mshiu amesema kuwa ili kuhakikisha wote wanafuata sheria na kujisajili, katika maonesho ya sabasaba wanaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma ndogo za fedha pamoja na sheria ya kanuni ndogo ya fedha ya mwaka 2018 na kanuni zake za mwaka 2019 ambazo zimeanza kutengenezwa mwaka 1920.
“Tangu mwaka 2021 taasisi yoyote ndogo ambayo inatoa huduma ya fedha ambapo anaendesha biashara hiyo bila kuwa na leseni ni kosa kwa mujibu wa sheria” amesema