NA STEPHANO MANGO, SONGEA
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Pius Chatanda anatarajia kufanya ziara ya kikazi Julai 7 mwaka huu katika kata za Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mjini ili kujiuonea uhai wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na kukagua miradi ya maendeleo
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Ofisini kwake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Mjini Mkoani Ruvuma James Mgego alisema kuwa Mwenyekiti wa Uwt Taifa Chatanda akiwa ameambatana na Wajumbe wa kamati ya Utekelezaji wa UWT Taifa watafanya ziara ya siku moja wilayani humo
Mgego alisema kuwa katika ziara hiyo Mwenyekiti Chatanda atakagua miradi inayotekelezwa na Chama pamoja na miradi inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya elimu, uchumi na miundombinu
Alisema kuwa akiwa Wilayani humo Mwenyekiti Chatanda atapata fursa ya kufanya vikao vya ndani na viongozi wa mashina, matawi na kata, pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na wananchi wa wilaya hiyo katika viwanja vya lizaboni
Mgego aliwataka viongozi na wananchi wote kujitokeza kwa wingi kumlaki mgeni huyo na kuhudhuria kwenye mikutano ya hadhara itakayohutubiwa na Mwenyekiti huyo na viongozi wa ngazi ya juu ya Jumuiya hiyo ya UWT Taifa
Alisema kwa namna ya pekee kabisa CCM Wilaya ya Songea Mjini inampongeza Rais Dkt Samia kwa namna anavyopambana kuhakikisha huduma za kiuchumi na kijamii zinawafikia wananchi, pamoja na ujenzi wa miundombinu ya elimu, usafirishaji
Naye Mwenyekiti wa Uwt Wilaya ya Songea Mjini Veneranda Nkwera alisema kuwa maandalizi ya kumpokea Mwenyekiti Chatanda kwenye kata zote ambazo amepangiwa kwenda yamekamilika na kwamba wanawake na wajasiriamali mbalimbali wanatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuja kusikiliza ujumbe aliokuja nao
Nkwera alisema kuwa Vikundi mbalimbali vya wajasiliamali vitakuwepo pamoja na burudani kutoka pande mbalimbali za Songea Mjini vitakuwepo kwenye shamra shamra za mapokezi hayo