Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula akizungumza wakati wa mkutano na Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) uliofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
…………………………………….
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi na mazingira ya kila siku ya utendaji.
Bi. Sara ametoa pongezi hizo alipokutana na Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Bw. Teophory Mbilinyi alipomtembelea ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuhudhuria kikao cha Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) uliofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Aidha Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka Bw. Teophory Mbilinyi ameupongeza uongozi wa TUGHE mkoa kwa kuendelea kuwa karibu na Tawi la TCAA kwani inatoa chachu ya uhai wa chama hicho.
Akizungumza wakati wa kikao, Mwenyekiti wa TUGHE tawi la TCAA Bi. Jacqueline Ngoda amewatia moyo wanachama kuendelea kujitoa kuwa mfano na viongozi kwa wengine ili kuwavuta wengi zaidi kujiunga na chama hicho.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Teophory Mbilinyi akizungumza na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula, Meneja Rasilimali Watu na Utawala Amina Silanda Ally pamoja na uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) walipotembelea ofisini kwake kwa ajili ya kutoa mrejesho wa mkutano wa Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la TCAA.
Meneja Rasilimali Watu na Utawala Amina Silanda Ally(mwenye ushungi) akizungumza na uongozi wa TUGHE Tawi la TCAA waliofika kutoa mrejesho kwa Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Teophory Mbilinyi wakati wa mkutano wa Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Teophory Mbilinyi(wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula (wa pili kushoto), Meneja Rasilimali Watu na Utawala Amina Silanda Ally(wa tatu kulia) pamoja na uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ukiongozwa na Mwenyekiti wa TUGHE tawi la TCAA, Jackline Ngoda(wa kwanza kushoto) pamoja na Katibu wa TUGHE tawi la TCAA, Shukuru Mhina (wa pili kulia) walipotembelea ofisini kwake kwa ajili ya kutoa mrejesho wa mkutano huo.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula akizungumza wakati wa mkutano na Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) uliofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Jackline Ngoda akimkaribisha mgeni rasmi Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula kwa ajili ya kuzungumza na Wajumbe wa TUGHE Tawi la TCAA kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Katibu wa TUGHE tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Shukuru Mhina akitoa taarifa za tawi hilo kwa mgeni rasmi Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula kwa ajili ya kuzungumza na Wajumbe wa TUGHE Tawi la TCAA kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula akiongoza Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kuimba wimbo wa mshikamano wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Sara Rwezaula (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakiongozwa na Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Jackline Ngoda (kushoto waliokaa) na Katibu wa TUGHE tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Shukuru Mhina (kulia waliokaa) wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo zilizopo Ukonga-Banana jijini Dar es Salaam.