Hamza Johari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) akizungumzana waandishiwa habari kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam kuhusu uhaba wa marubani nchini.
Hamza Johari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) akielekeza jambo kwa wafanyakazi wa shirika hilo kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam kuhusu uhaba wa marubani nchini.
Hamza Johari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam kuhusu uhaba wa marubani nchini.
………………………………………………….
Uhaba wa Marubani nchini umekuwa chanzo cha Kuwepo Kwa Mfuko wa Mafunzo ili kupata marubani wazawa watakaotosheleza soko la nchi.
Akizungumza Leo Julai 5 kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam Hamza Johari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) amesema wameanza kusomesha marubani ili kupunguza changamoto waliyonayo ya uhaba wa marubani hasa wazawa Kwani pesa za kuwalipa marubani ni nyingi na marubani waliopo ni wachache Hali inayopelekea rubani kufanya kazi zàidi ya kampuni Moja.
“Katika sekta yetu tunachangamoto kubwa mbili ambazo ni uhaba wa marubani pamoja miundombinu ya viwanja vya ndege katika kuliona Hilo tumeanzisha mfuko wa mafunzo ili wakimaliza waajiliwe na kupunguza changamoto hiyo,”.amesema Hamza Johari
Aidha Hamza Johari Amesema kuwa wananchi Kwa kutopenda somo la hesabu ndio imekua chanzo Cha upungufu wa marubani hivyo wameanzisha klabu za wanafunzi ili kuwajengea uwezo.
Sambamba na hayo amesema wamevifungia viwanja vya ndege 300 Kwa kutokua na vigezo vya kurukia ndege viwanja hivyo hasa ni vile vilivyopo kwenye mapoli.
Ameongeza kuwa (TCAA) ndio wenye mamlaka ya kusimamia ujenzi wa viwanja vya ndege pia na huduma za ardhini zikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za chakula na ujazaji wa mafuta.
“Kuna makampuni yanatoa huduma za adhini kama swissiport sisi ndio tunawapa kibari Cha kutoa huduma hizo”amesema……
Aidha ameongeza kuwa (TCAA) wanatoa leseni kwa ndenge nyuki(droni)ambapo mtoa huduma hiyo anapaswa kuwa amesajiliwa na kupatiwa leseni.
Mamlaka ya usafiri wa anga TCAA mpaka Sasa wanasimamia anga lote la Tanzania na Rwanda.