Prof. Patrick akizungumza wakati wa mjadala wa wazi kuhusu “Kiswahili Nyenzo ya Ukombozi wa Fikra kwa Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika” ikiwa ni Kuelekea Kilele cha Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7, 2023.
……
Na Eleuteri Mangi, WUSM, Zanzibar
Prof. Patrick Lumumba amesema ukitaka kuelewa lugha ni lazima kutambua muktadha wake na Kiswahili ni kitega uchumi kinajitosheleza kisayansi kwa maendeleo ya watumiaji wa lugha hiyo.
Prof. Lumumba amesema hayo Julai 5, 2023 Zanzibar wakati wa mjadala wa wazi kuhusu “Kiswahili Nyenzo ya Ukombozi wa Fikra kwa Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika” ikiwa ni Kuelekea Kilele cha Siku ya Kiswahili Duniani Julai 7, 2023.
“Kiswahili ni lugha ya Kiafrika, ni nyenzo pekee ya kuwakomboa Waafrika, kinatuunganisha sisi sote Waafrika, tujivunie Siku ya Kiswahili Duniani” amesema Prof. Lumumba.
Kwa upande wake Prof. Amani Lusekelo Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema Taasisi za Elimu ya Juu nchini zinawajibu wa kupanua hadhi ya lugha ya Kiswahili kwa kuandika tasnifu kwa lugha ya Kiswahili.