Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) Bw. Ahmad Abdallah akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) Bw. Ahmad Abdallah akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Shirika hilo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Amanieli Lyimo Kaimu Meneja Mauzo na Masoko NHC.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) Bw. Ahmad Abdallah akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) Bw. Ahmad Abdallah akiakiangalia makala fupi inayoelezea miradi ya NHC inayotekelezwa na shirika hilo nchini wakati alipotembelea banda la shirika hilo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) Bw. Ahmad Abdallah akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa NHC hilo wakiwa katika banda la shirka hilo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
………………………………………………………..
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limejipanga kuendelea kutekeleza miradi kwa ufanisi ikiwemo Samia Scheme ambao unalengo la kujenga Nyumba 5,000 katika Mikoa mbalimbali yenye soko na uhitaji.
Akizungumza leo tarehe 5/7/2023 Jijini Dar es Salaam na waandishi wa Habari katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) Bw. Ahmad Abdallah, amesema kuwa kupitia Samia Scheme Shirika limezamilia kuwasaidia watanzania kuwajengea Nyumba kwa gharama nafuu.
Amesema kuwa mradi wa Samia Scheme una nyumba bora na gharama nafuu ukilinganisha na thamani halisi ya nyumba hizo.
“Kuna Studio Apertment ina chumba kimoja, sebure, choo na jiko ambapo inauzwa shilingi milioni 37” amesema Bw. Abdallah.
Amesema kuwa gharama za nyumba hizo ni nafuu kwani ni vigumu kupata kiwanja, nyumba ya chumba kimoja katika maeneo ya Kawe ambayo yapo karibu na bahari.
Amesema kuwa watanzania wameendelea kuchangamkia fursa katika mradi wa Samia Scheme ambapo wamejenga nyumba 560 na mpaka sasa asilimia 81 tayari nyumba hizo zimeuzwa.
Amefafanua kuwa mradi wa Samia Scheme una nyumba 5,000 ambapo nyumba nyengine wanatarajia kujenga katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Arusha katika maeneo yenye uhitaji na soko.
“Tunatakiwa kujiendesha kibiashara, miradi yetu mingine tunakopa na ili tuweze kurejesha fedha lazima tuuze, tunaendelea kufanya uchambuzi wa maeneo ili kubaini yenye uhitaji na soko” amesema Abdallah.
Bw. Abdallah amesema kuwa asilimia 10 ya nyumba za mradi wa Samia Scheme tayari zimejengwa Mkoa wa Dar es Salaam, na wanatarajia kuanza awamu ya pili kwa kujenga nyumba 500 katika mikoa yenye uhitaji.
Akizungumzia Nyumba za Kariakoo ambapo zina wapangaji, ameeleza kuwa tayari wamekubaliana na wapangaji hao kuhama kwa ajili ya kumpisha mbia kwa ajili ya kufanya maboresho.
“Haki za wapangaji wetu zipo katika mikataba yetu ambayo tulikubaliana nao, tunachokifanya sasa hivi ni kuangalia jicho la kibinadamu ambapo tumeongeza muda hadi miezi saba ya kukaa” amesema Bw. Abdallah.