Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Bi. Zuhura S. Muro akisaini kitabu cha Wageni baada ya kuwasili katika banda l Shirika hilo alipotembelea maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini DSM.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Bi. Zuhura Muro akipata maelezo kuhusu Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara Bw.Vedastus Mwita alipotembelea banda la TTCL katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini DSM.
Akipata maelezo kuhusu huduma ya Publi wifi inayotolewa na TTCL na kufanikisha kuonekana live kwa shughuli za kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro.
…………………………..
Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL limeendelea kujivunia matunda yatokanayo na ukuaji wa Teknolojia ambapo hivi Sasa imekua ikitangaza utalii kidigitali.
Akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya biashara ya 47 jijini Dar es salaam July 3 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo Sinare Muro amesema ukuaji huo wa Teknolojia umepelekea kukuza sekta ya utalii Kwani unaweza kumshuhudia mtalii akiwa kwenye vivutio mbalimbali mubashara Kwa kutumia mfumo wa kisasa iliyopo katika shirika.
Amesema shirika linafungua nchi katika uchumi wa kidigital Kwani Sasa wanauweza wa kuendesha vituo vya mawasiliano (Call Center) ambavyo vimefungwa kwenye taasisi mbalimbali kote nchini.
“Ukuaji huu wa Teknolojia kwetu sisi kama TTCL unatusaidia kuifungua nchi ukiacha kutangaza utalii kidigitali lakini pia tunaweza kuunganisha nchi lakini hata kuuza ubunifu wa Teknolojia tuliyonayo”ameongeza Muro
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga amesema wamekuja na huduma ya kuwafikishia huduma ya mtandao wananchi mpaka nyumbani.
“Sasa hivi tunahakikisha uchumi unakua kidigital ndio maana tumekuja na mpango wa kufikisha huduma ya mtandao mpaka nyumbani ifahamikayo kama Fiber Mlangoni hii ni rahisi na itasidia Kila mwananchi anayetumia mtandao katika shughuli zake za Kila siku”amesema Ulanga.