Ni tukio la Utalii kwa watoto na wazazi/walezi wao kipindi cha likizo ikiwa na lengo la kukuza Utalii wa Ndani na kuwavisha ubalozi wa Utalii watoto ambao ndio tegemeo la baadae katika kuiongelea na kuikuza sekta ya Utalii nchini.
Aidha Wajukuu wa Mama Royal Tour inabeba agenda muhimu ya kuunga mkono jitihada za Mh Raisi Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza Utalii kimataifa kupitia filamu maarufu ya The Royal Tour.
Wajukuu wa Mama Royal Tour kwa safari hii wametembelea Hifadhi ya Mikumi ikijumuisha jumla ya watoto 70 ambapo 20 wametoka kwenye vituo Maalumu vya kulelea watoto wakiokngozwa na Walimu, Wazazi na Walezi wao.