Chuo Cha VETA Pwani kinajivunia mradi mpya wa mashine ya kutengenezeza, kudalizi na kufuma nembo au maumbo mbalimbali Katika nguo kwa kutumia kompyuta ambayo yatawekwa kwenye mashine yoyote
Akizungumzia kuhusu mradi huo, mwalimu kutoka katika Chuo hicho Necsory Kayombo amesema wao hufundisha mwanafunzi kutengeneza nembo au maua mbalimbali ya pembeni na kuweka kwenye mashine ambayo inafanya kulingana na ulivyoielekeza.
“Kwa mfano inavyoonekana hapa hii nembo ambayo tayari imeshatengenezwa unaweza ukaweka kebo au flashi na kuiamishia kwenye mashine ambayo huku unapanga kabisa Uzi na upande huu mwingine zinapangwa kwa namba, inafanya kazi mpaka ikimaliza Uzi au ikikata Uzi au ikimaliza kazi.
“Machine hizi zinapatika Nchi tofauti tofauti lakini sisi hii tumechukua Korea hivyo tunaandaa nguvu kazi ambayo itasaidia Kijana kwenda kuajiriwa au kujiajiri,” amesema Kayombo
Kozi nyingine zitolewazo katika Chuo hicho Cha veta Pwani ni pamoja na ushonaji kuanzia levo 1 mpaka 3,Umeme wa magari na WA majumbani,maabara pamoja na sekretari.