Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali, Maspika, Naibu Maspika pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 53 wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha 03 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson mara baada ya kuwasili Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa 53 wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha 03 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati akielekea kushiriki na kufungua Mkutano Mkuu wa 53 wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha 03 Julai, 2023.
Wajumbe wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) wakiwemo Maspika, Naibu Maspika, Wabunge pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa 53 wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha 03 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Maspika, Naibu Maspika pamoja na wajumbe wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-PF) mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 53 wa Jukwaa hilo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha 03 Julai, 2023.
……..
Julieth Laizer,Arusha .
Arusha.Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa, serikali imejiwekea mikakati ya kuwashirikisha Vijana katika sekta ya Kilimo ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chakula.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha katika ufunguzi wa kikao cha 53 cha Jukwaa la mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo amesema ili kuwepo na usalama wa chakula katika SADC ni muhimu kushirikisha vijana katika Kilimo.
Amesema Tanzania imeanza mkakati huo ambao unajulikana kama Building better tomorrow (kuwajenga kesho iliyobora)mkakati ambao unatarajiwa kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo na kuongeza Mnyororo wa thamani katika mazao ya Kilimo.
Rais Samia amesema, mkakati huo licha ya kusaidia kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali lakini pia utasaidia kukuza ajira kwa vijana hadi kufikia 1,500,000.
Amesema Tanzania pia imekuwa ikitekeleza kwa kiasi kikubwa Azimio la Maputo la kutenga asilimia 10 ya bajeti katika sekta ya Kilimo ambapo Sasa kiasi kinachotengwa kimefikia zaidi ya Sh 1 trilioni .
Amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo ni muhimu wabunge kwa kushirikiana na serikali kuongeza ushiriki wa vijana ambao ni wengi kupenda .
Kwa upande wake SPIKA wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk.Tulia Hassan amesema kuwa ,Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wamekusanyika jijini Arusha kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo uwekezaji katika eneo la kilimo huku lengo kuu likiwa ni kuhakikisha wanataka kilimo kiwe cha kisasa .
Dk.Tulia amesema , lengo kuu la kukutana mabunge hayo ni kuhakikisha Tanzania katika nchi za Afrika inajitosheleza kwa chakula na kutoa ajira kwa vijana.
“Hiki ni kikao cha 54 na ni mara ya nne kufanyika hapa nchini Tanzania kukusanya mabunge haya tunataka kuhakikisha Tanzania na jumuiya ya nchi za Afrika inajitosheleza kwa chakula.”amesema Dk.Tulia.
Amesema ,wanataka kuona vijana wengi wanajiwekeza katika eneo hilo na kuhakikisha wanajiajiri katika sekta hiyo ya kilimo kwani ni sekta ambayo inaajiri idadi kubwa ya watanzania .
“Tuna amini mabunge kutoka nchi za Afrika watakuja kujifunza kutoka kwetu na sisi tuweze kuwa mfano wa kuigwa na nchi zingine na tumekutana mabunge kwani sisi ndio tunapitisha bajeti lakini pia ndio tunaishauri serikali .”amesema
Ameongeza kwa kusema, sasa hivi nchi ya Tanzania tumeanza kupiga hatua na fedha nyingi zimewekezwa katika eneo hilo na wadau mbalimbali kujitokeza kuwekeza katika sekta hiyo lengo likiwa ni kuhakikisha kuna uwekezaji wa kutosha katika sekta hiyo.
Amesema ,kwa sasa hivi Tanzania wanafanya vizuri sana na wanaweza kulisha Tanzania na dunia nzima kwa ujumla.
Mkutano huo wa siku Saba unashirikisha wabunge wa SADC kutoka Zimbabwe,Namibia,Sherisheri,Afrika Kusini, Lesotho,Malawi, Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Eswatini,Angola, Botswana,Zambia, na wenyeji Tanzania.