Mratibu wa Mafunzo Chuo cha Benki Kuu Mwanza, Tula Mwigune akizungumza kuhusu kozi mbalimbali ziazotolewa kwenye chuo cha Benki Kuu ya Tanzania jijini Mwaza kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
………………………………..
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Chuo Cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kilichopo Mkoani Mwanza kinawakaribisha wanafunzi kujiunga na chuo hicho kwa ajili ya kupata mafunzo ya masuala mbalimbali ya biashara na benki.
Akizungumza leo tarehe 2/7/2023 katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Kibiashara Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Mafunzo Chuo cha Benki Kuu Mwanza, Tula Mwigune, amesema kuwa mwaka 2020 chuo kilianza kutoa mafunzo ya masuala ya benki kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita.
Mwigune amesema kuwa kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne anapaswa kuwa na cheti cha masuala ya biashara ili aweze kujiunga na masomo.
“Tunatoa kozi ya masula ya benki ngazi ya Diploma kwa muda wa miaka miwili katika Chuo Chetu Cha BoT Mwanza” amesema Mwigune.
Amesema kuwa dirisha la maombi la kujiunga na Chuo limefunguliwa, hivyo mtu yoyote anaweza kutuma maombi moja kwa moja kupitia mfumo wa chuo.
Amefafanua kuwa pia Chuo kinapokea wanafunzi waliomaliza elimu ya juu ambao wanapenda kusoma kozi ya masuala ya Benki.
“Tunatoa kozi ya Post graduate in Bank Manegment kwa wanafunzi waliomaliza elimu ya juu ambao wamesomoa kozi tofauti na masuala ya banki na walikuwa la lengo la kufanya kazi katika taasisi za fedha” amesema Mwigune.
Amesema kuwa programu hiyo inafundishwa kwa muda wa miezi tisa ambapo miezi sita darasani na miezi mitatu wanafanya mazoezi ya vitendo.
Mwigune ameeleza kuwa dirisha la maombi ya kujiunga na chuo litafungwa tarehe 28/7/2022 kwa awamu ya kwanza na mwezi Agosti wanatarajia kufungua tena kwa ajili ya awamu ya pili, huku akibainisha kuwa masomo yanatarajia kuanzia mwezi Oktoba 2023.
Chuo Cha BoT kimeanzisha mwaka 1991 kwa malengo ya kutoa elimu kwa wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) lakini kadri muda unavyozidi kwenda waliona umuhimu wa kutoa elimu kwa wafanyakazi wa taasisi za fedha.
Chuo kiliendelea kutoa huduma kwa wafanyakazi ambao wapo ndani na nje ya nchi ikiwemo nchi za Afrika Mashariki.
……………………………………………………………………
PITIA MAELEZO HAPA CHINI ILI KUJUA NAMNA UNAVYOWEZA KUJIUNGA NA KOZI MBALIMBALI ZA CHUO HICHO
ORDINAYR DIPLOMA
Chuo cha Benki kuu ya Tanzania yaani Bank of Tanzania Academy kilichopo Capripoint
Jijini Mwanza ni chuo chenye ithibati ya baraza la taifa la elimu ya ufundi na mafunzo ya
ufundi stadi yaani NACTVET, chuo kinatoa Stashahada ya taaluma ya kibenki na
usimamizi wa mabenki yaani Ordinary Diploma in Banking Practice and Supervision.
Mkuu wa chuo anawakaribisha wanafunzi wenye sifa zifuatazo kutuma maombi ya
kujiunga na diploma katika campus ya Mwanza; ufaulu wa angalau principal pass moja
na subsidiary pass moja kwa kidato cha sita au cheti cha ufundi daraja la nne National
Technical Award Level 4 katika taaluma ya biashara kutoka chuo kinachotambuliwa na
NACTVET.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22 September 2023 na masomo yataanza rasmi
mwezi October 2023.
Ada zetu ni nafuu kabisa. Maombi yanapokelewa kupitia mfumo wa maombi ambao ni
https://oas.botac.ac.tz.
Kwa mawasiliano Zaidi piga simu nambari 0769 085 002 au 0713 820 394
Kwa utaalamu mahiri katika fani za kibenki karibu Chuo cha Benki Kuu Mwanza.
POSTGRADUATE DIPLOMA
Chuo cha Benki kuu ya Tanzania yaani Bank of Tanzania Academy kilichopo Capripoint
Jijini Mwanza ni chuo chenye ithibati ya baraza la taifa la elimu ya ufundi na mafunzo ya
ufundi stadi yaani NACTVET, chuo kinatoa stashahada ya udhamili katika uongozi wa
benki yaani Postgraduate Diploma in Bank Management, program hii inatolewa kwa
ushirikianao na chuo cha usimamizi wa fedha IFM.
Mkuu wa chuo anawakaribisha waombaji wenye sifa kujiunga na masomo ya
stashahada ya uzamili yaani Postgraduate Diploma in Bank Management
yanayoendesha katika vyumba vya mafunzo vilivyopo benki kuu makao makuu ndogo
Dar es Salaaam. Course hii inaendesha kwa muda wa jioni yaani evening programme
kwa kipindi cha miezi tisa tuu yaani miezi sita darasani na miezi mitatu ya utafiti na
andiko.
Sifa za kujiunga na programme hii ni shahada ya kwanza yaani bachelor degree au
stashahada ya juu advanced diploma kutoka chuo kinachotambulika na serikari.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22 September 2023 na masomo yataanza rasmi
mwezi October 2023.
Ada zetu ni nafuu kabisa. Maombi yanapokelewa kupitia mfumo wa maombi ambao ni
https://oas.botac.ac.tz.
Kwa mawasiliano Zaidi piga simu nambari 0769 085 002 au 0713 820 394
Kwa utaalamu mahiri katika fani za kibenki karibu Chuo cha Benki Kuu Mwanza.
COMBINED
Chuo cha Benki kuu ya Tanzania yaani Bank of Tanzania Academy kilichopo Capripoint
Jijini Mwanza ni chuo chenye ithibati ya baraza la taifa la elimu ya ufundi na mafunzo ya
ufundi stadi yaani NACTVET, chuo kinatoa stashahada ya taaluma ya kibenki na
usimamizi wa mabenki yaani Ordinary Diploma in Banking Practice and Supervision na
stashahada ya uzamili katika uongozi wa benki yaani Postgraduate Diploma in Bank
Management.
Mkuu wa chuo anawakaribisha waombaji wenye sifa kujiunga na masomo ya diploma
yanayoendesha katika campus ya Mwanza na Postgraduate Diploma yanayoendesha
katika vyumba vya mafunzo vilivyopo benki kuu makao makuu ndogo Dar es Salaaam.
Sifa za kujiunga na programme ya Diploma ni angalau ufaulu wa principal pass moja na
subsidiary pass moja kwa kidato cha sita au cheti cha ufundi daraja la nne National
Technical Award Level 4 katika taaluma yoyote ya biashara kutoka chuo
kinachotambuliwa na NACTVET.
Na kwa Postgraduate Diploma ni shahada ya kwanza yaani bachelor degree au
stashahada ya juu yaani advanced diploma kutoka chuo kinachotambulika na serikari.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 22 September 2023 na masomo yataanza rasmi
mwezi October 2023.
Ada zetu ni nafuu kabisa. Maombi yanapokelewa kupitia mfumo wa maombi wa chuo
ambao ni https://oas.botac.ac.tz.
Kwa mawasiliano Zaidi piga simu nambari 0769 085 002 au 0713 820 394
Kwa utaalamu mahiri katika fani za kibenki karibu Chuo cha Benki Kuu Mwanza.
COURSE ZA MUDA MFUPI
Chuo cha benki kuu kinatoa pia course za muda mfupi kwa watu waliopo katika taasisi
za fedha. Lengo la course hizi ni kuwapa ujuzi na kuongeza ufanisi wa utendaji wao wa
kazi. Ratiba ya course hizo inatoka kila mwaka mwezi wa kumi na moja na inapatikana
katika website ya chuo ambayo ni academy.bot.go.tz.
Mratibu wa Mafunzo Chuo cha Benki Kuu Mwanza, Tula Mwigune akizungumza na wananchi mbalimbali waliotembelea katika banda la Benki Kuu ya Tanzania BoT kwenye Maonesho ya 47 ya biashara ya Kimataifa yanayofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi na watoto mbalimbali wakipata maelezo walipotembelea katika banda la Benki Kuu ya Tanzania BoT.