NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, inatekeleza mradi wa miaka mitano wa Kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) ulionza mwaka 2020.
Tasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imepewa jukumu la kuimarisha utolewaji wa Programu ya Elimu ya Sekondari kwa njia Mbadala (SEQUIP-AEP) kwa wasichana waliokatisha masomo ya elimu ya sekondari kwa sababu mbalimbali.
Lengo kuu la Mradi ni kuimarisha ubora wa elimu ya Sekondari inayotolewa kwa njia mbadala, kuboresha uhitimu bora wa elimu ya Sekondari kwa walengwa pamoja na kuwapatia wasichana mazingira bora ya kujifunzia.
Pia kuongeza ufikiwaji wa wasichana walioshindwa kuendelea na elimu ya Sekondari kwa sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa, hali duni ya maisha au kupata ujauzito ambapo mradi umelenga kuwafikia wasichana wapatao 12,000 nchini kote.
Walengwa wa mradi ni wasichana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 20 waliokatisha masomo ya elimu ya programu ya elimu ya Sekondari kwa sababu mbalimbali.
Mradi unatoa fursa kwa mara nyingine kwa wasichana kuweza kuendelea na masomo ya elimu ya Sekondari ambapo Serikali inagharamia malipo ya Ada na hatimaye kufikia malengo waliyojiwekea.
Licha ya Serikali kutoa Fursa kwa Wasichana waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali kuendelea na Masomo kupitia mradi SEQUIP bado kuna baadhi ya Mabinti waliopata nafasi hiyo wanakatiza masomo huku miongoni mwa sababu zinazotajwa hali duni ya Maisha.
Hayo yamejiri Mkoani Morogoro kwenye Warsha ya kuwajengea uwezo Walimu 75 wa Masomo ya Sanaa na Lugha wanaofundisha Wanafunzi waliokatiza Masomo na kurudi shule kutoka mikoa 14 Tanzania Bara kupitia Mradi SEQUIP.
Mratibu wa Mradi wa SEQUIP Kitaifa kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu wazima, Bw. Baraka Kionywaki amesema Wanafunzi 604 kati ya 3333 wameshindwa kuendelea na masoma licha ya kurudi shule baada ya kupitia kadhia na kushindwa kufanya Mitihani ya Kitaifa.
“Kuna wanafunzi kwa namna moja au nyingine wananshindwa tena kuendelea na Masomo, wanakuwa na Utoro rejareja, sugu na wapo wengine ambao kwa bahati mbaya sana tunasikitika wanakatisha Masomo.” Alisema
Amesema kukatishwa kwa Masomo kwa wananfunzi hao kunasabaishwa na baadhi ya Wazazi kuwa na hali ngumu ya uchumi, kuwafanya watoto kike kuwa chanzo cha kipato katika Familia.
“Wengi wamekuwa wakishindwa kuendelea na Masomo sio kama hawataki, lakini Mazingira magumu ya nyumbani analazimika kufanya Biasgara ndogondogo na wengine kufanya kazi za ndani”.
Alisema Mratibu.
Ameseama katika kutatua changamoto hizo kupitia Mradi wa SEQUIP, Serikali imetenga Shilingi Bilioni 5 kwaajili kuweka Mazingira rafiki ya Wanafunzi hao kuweza kusoma.
“Katika vituo tulivyovijenga kupitia mradi wa SEQUIP, tumeweka vyumba Maalumu kwajili ya kunyonyesha watoto, pia tumemuajiri mtu ambaye anawatunza watoto wakati mama zao wakiwa Darasani wanaendelea na Masomo” alisema Mratibu
Serikali kwa kushirikiana na Asasi nyingine, katika kutatua changamoto ya mabinti kushindwa kuhudhulia masomo katika vituo vilivyopangwa kwa sababu ya mbalimbali hususani hali duni ya maisha imejenga Mabweni karibu na vituo.
Mkuu wa Kampasi ya Taasisi ya Elimu ya Watu wazima Morogoro Dkt. Honest Kipasika amewataka walimu wanaofundisha wanafunzi waliokataza masomo wanatakiwa kuwa na mbinu nyingi mbadala kwani wanawafundisha watu waoliopitia kadhia mbalimbali.
Kwa upande wao walimu wa Masomo ya Sana na Lugha waliopata mafunzo hayo wamesema yatawasaidia katika utendaji kazi wao pamoja na kutatua changamoto za wanafunzi.