………………….
Dar es Salaam,
Jeshi la Polisi nchini limesema limeimarisha usalama katika maonesho ya sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam ili wafanyabiashara waweze kufanya kazi zao kwa amani na utulivu na kukuza biashara zao.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime wakati akielezea lengo la Jeshi hilo katika viwanja vya maonesho Sabasaba.
Msemaji wa Jeshi la PolisiMaonesho hayo yaliyoanza Juni 28 yanaendelea ambapo Taasisi, Idara na wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi wanaonesha na kutoa huduma mbalimbali.