Mwanafunzi Patrick Ezekiel Patrick akionesha mtambo wa kufua umeme uliobuniwa kwa ajili ya kufundishia wananunzi katika chuo cha VETA cha Dodoma.
…………………………….
Na John Bukuku.
Chuo Cha Ufundi Stadi VETA Kampasi ya Dodoma Kimebuni mfumo wa uzalishaji umeme unaotumia maji.
Mfumo huo ambao ni maalum kwa kufundishia wanafunzi ni sehemu ya maonyesho yanayopatikana katika Banda la VETA ambapo kila mwaka huja na kitu kipya ikiwa ni sehemu ya ubunifu ya maonyesho ya 47 ya kimataifa ya wafanyabishara
Akizungumza katika maonyesho ya 47 ya Kimataifa ya biashara ya 47 yaliyoandaliwa na TANTRADE katika viwanja vya sabasaba Mwanafunzi Patrick Ezekiel Patrick amesema mfumo huo ndio mfumo halisi wa maji unatumika kuzalisha umeme.
Amesema mfumo huo ameubuni yeye kwa kushirikiana na mwalimu wake wa masomo.
“Katika maonyesho ya mwaka huu sisi Kama VETA tumekuja na mfumo wa uzalishaji umeme unatumia maji,huu mfumo Kama unavyouona hapa ndio mfumo unatumika katika kuzalisha umeme wa maji”, amesema Patrick
Amesema mwananchi au Mwanafunzi atakayefika katika Banda la VETA ataweza kujionea namna umeme unavyozalishwa ,jinsi unavyosafirishwa mpaka kufikia sehemu ya kupozea umeme na kuweza kutumika.
Amesema katika mfumo huo Kuna Jenereta linalotengeneza mzunguko kutokana na kasi ya maji pia Kuna transfoma , Socket ambapo vyote hivyo ndio vinavyotumika katika kuzalisha umeme wa maji.
Aidha amewataka vijana kuendelea kujiunga na VETA ili kuweza kutimiza malengo yao ya baadaye
Hata hivyo ameushukuru uongozi wa VETA kwa kuwapa ujuzi unaowasaidia kuweza kujiajiri wenyewe