Meneja mkuu msaidizi wa Usalama wa Raia Saccos,URA ,Mrakibu mwandamizi wa polisi,Peter Msuya akizungumza jambo na waandishi wa habari.
Baadhi ya viongozi wa chama cha Usalama wa Raia Saccos,URA wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Lucas Raphael,Tabora
Usalama wa Raia Saccos,URA imetoa Zaidi ya Shilingi 458 bilioni zimekopeshwa kwa wanachama wake tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006.
Kiasi hicho kimetokana na jumla ya mikopo 114,015 iliyotolewa kwa wanachama wake ambao wamenufaika na chama hicho.
Meneja mkuu msaidizi wa Ura,Mrakibu mwandamizi wa polisi,Peter Msuya akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani,SUD,alisema mikopo hiyo imewawezesha wanachama wake kujenga nyumba, kusomesha, kununua vyombo vya usafiri na mengine mengi.
“Mikopo iliyotolewa kwa wanachama mbali ya kuwawezesha kufanya mambo mbalimbali pia imekuza uchumi na kuongeza mzunguko wa fedha nchini,”amesema
Alieleza kuwa Saccos hiyo yenye wanachama wapatao 45,000 ina rasilimali za Shilingi Bilioni 117 na kupata tuzo za ubora za uendeshaji wa chama na kwamba misingi ya ushirika inaweza kuwakomboa watu.
Kwa mwaka jana 2022,Saccos hiyo imetoa mikopo 17,458 yenye thamani ya Shilingi billion 108.7 kiwango ambacho ni kikubwa kutolewa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006.
Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa ,Dk Batilda Burian,Dkt Rashid Chuachua ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Kaliua,alipongeza Saccos hiyo kwa kutoa mikopo kwa watumshi wa jeshi la Polisi na Askari.
Alisema kwamba jeshi la polisi kipitia saccos hiyo limefanya jambo jema la kuhakikisha linaendelea kutoa mikopo ya maramara kwa mara ili asakari wote wanaufaike nayo.
Mkuu huyo wa wailaya alisema kwamba maadhimisho hayo kufanyika mkoa wa Tabora kwa mara ya tatu mfululizo na kwamba yanaongeza mzunguko wa fedha.
“Mkoa umenufaika kufanyika maadhimisho kwa mara nyingine na wananchi kunufaika kiuchumi,”alisema
Katika maadhimisho hayo yanayotarajia kufungwa Julai 1,2023,yanahudhuriwa na wadau mbalimbali wa ushirika na kuwa na mabanda yapatayo 250.