Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba akiuliza jambo Kwa Crispina Nkya Afisa Mwandamizi Mkuu Usimamizi wa Safaru BoT wakati alipotembelea Katika Banda la Benki hiyo kuona Elimu inayotolewa Kwa Umma kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Benki hiyo kwenye maonesho ya Biashara ya 47 yaKimataifa TANTRADE yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Leo Ijumaa 29, Juni, 2023 kulia ni Elirehema Msemembo Mhasibu Mkuu Mwandamizi BoT.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-SABASABA)
………………………………………..
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imesema itaendelea kusimamia sera za fedha ili kuhakikisha kunakuwa na mwelekeo mzuri wa uchumi jambo ambalo litasaidia shilingi kuendelea kuwa imara na kuleta Tija kwa Taifa.
Akizungumza leo tarehe 29/6/2023 jijini Dar es Salaam wakati akitembelea la Benki Kuu ya Tanzania BoT katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Emmanuel Tutuba, amesema kuwa shilingi ya Tanzania imeendelea kuwa na imara ukilinganisha na sarafu za nchi nyengine.
Tutuba amesema kwa miaka 10 iliyopita sarafu ya Tanzania imeshuka Kwa asilimia 1.4 na kuwa miongoni mwa sarafu chache duniani ambazo zipo imara katika uchumi.
Amesema kuwa Benki Kuu imeendelea kusimamia sera ya fedha na kutengeneza mazingira rafiki ili kuhakikisha kunakuwa na mzunguko mzuri wa fedha na kudhibiti mfumuko wa bei katika soko.
“Fedha zote zipo serikalini, unaweza kuzitoa fedha na kupeleka katika taasisi mbalimbali, kwa wananchi kupitia mishahara, miradi mbalimbali kwa lengo la kuweka sawa mzunguko wa fedha” amesema Tutuba.
Amefafanua kuwa kuwa sera za kifedha ni kama damu katika mwili, hivyo hivyo ili shughuli za uchumi ziendelee kukua lazima kuwe na fedha “Uwiano katika mzunguko wa fedha inapaswa kuendana na kiwango cha uzalishaji”
Amesema kuwa shughuli za uzalishaji na shilingi zinategemeana hivyo uwepo wa huduma za biashara na kufanya miamala inazuia mfumuko wa bei na kuendelea kuwa na sera madhubuti kwa nchi.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba akitoa maagizo Kwa Crispina Nkya Afisa Mwandamizi Mkuu Usimamizi wa Safaru BoT na Elirehema Msemembo Mhasibu Mkuu Mwandamizi BoT kulia wakati alipotembelea Katika Banda la Benki hiyo kuona Elimu inayotolewa Kwa Umma kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Benki hiyo kwenye maonesho ya Biashara ya 47 yaKimataifa TANTRADE yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam Leo Ijumaa 29, Juni, 2023.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba akiangalia alama za usalama katika noti za elfu kumi na elfu tano wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye Maonesho ya Biashara ya 47 Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba akitembelea maeneo mbalimbali katika banda hilo.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba akikagua eneo lililohifadhiwa Noti mbalimbali na sarafu kwa ajili ya kuonesha wananchi katika maonesho hayo.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba akitoa maagizo kwa Nestory Maro Mchambuzi wa Mifumo ya Malipo Benki Kuu ya Tanzania BoT wakati alipotembelea Kurugenzi inayoshughulikia mifumo ya kifedha.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bw. Emmanuel Tutuba akiangalia jarida lililochapishwa sarafu mbalimbali zilizotumika tangu enzi za wakoloni na ambazo zinatumika sasa.
Picha mbalimbali zikionesha wananchi wakitembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania BoT katika maonesho hayo kwenye viwanja vya sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.