Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Karimu Meshack akionesha nembo ya tuzo ya Superbrands ambayo Shirika hilo limetunukiwa mwaka huu kutokana na maboresho makubwa waliyoyafanya katika soko la utoaji wa huduma za Bima katika ukanda wa Afrika Mashariki.
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Shirika la Bima la Taifa (NIC) limeshinda Tuzo ya Superbrands Afrika Mashariki na kukidhi vigezo vya Kimataifa na kupata Cheti cha Ithibati cha utoaji wa huduma bora za Bima.
Hatua hiyo imekuja baada ya NIC kufanya uwekezaji kwa wataalam, mitambo ya kisasa kwa kutoa huduma ya kidijitali kwa kutumia mifumo ya Tehama.
Akizungumza leo tarehe 29/6/2023 Jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw. Karimu Meshack, amesema kutokana na uwekezaji uliofanyika katika kipindi cha miaka minne wamepata faida zaidi ya asilimia 100.
Bw. Meshaki amesema katika mwaka 2022 wamepata faida ya shilingi bilioni 63 .2 sawa na asilimia 108 na kuvunja rekodi kwani hakuna Kampuni yoyote ya bima iliyopata faida hiyo nchini Tanzania.
Amesema kuwa uwekezaji wa mifumo ya utoaji wa huduma imechangia kwa asilimia kubwa kupata Tuzo ya Superbamds Afrika Mashariki.
Bw. Meshack amesema kuwa sasa wameboresha utoaji wa huduma kwani wameweza kuwalipa wateja madai yao ndani ya siku saba kwani awali walikuwa wanalipa katika kipindi cha siku 45.
“Uboreshaji wa huduma unawafanya wateja wetu kufurahia huduma kwani kwa muda mfupi wanapata majibu” amesema Bw. Meshaki.
“Na ndiyo maana tunasema sisi ndiyo Bima Mwaka huu Oktoba 16 tunafikisha miaka 60 ya utoaji wa huduma za bima hivyo sisis ni Wazoefu, Wazeefu na Wabobezi katika utoaji wa huduma za bima nchini Tanzania kutokana na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwa muda mrefu,”. Amemalizai Bw. Karimu Meshack