………………..
Na. Sixmund J. Begashe
Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na wageni kutoka Mataifa Mbalimbali wamemiminika katika Banda la Maliasili na Utalii lililopo kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam katika Sikuku ya Eid Ili kujifunza na kuburudika kupitia maonesho ya Taasisi za Wizara hiyo.
Akizungumza baada ya kutembelea Banda hilo la Maliasili, Makazi wa Kimara Baruti Bw. Juma Ally amesema, ameona vyema awatembeze watoto wake kwenye Maonesho hayo ili waweze kukamilisha furaha yao ya Sikuku ya Eid kwa kuona Wanyama mbalimbali, Nyumba ya asili, kujifunza kuhusu Misitu, Utalii, Nyuki na huduma mbalimbali zinazo tolewa na Wizara hiyo.
Bw. Juma licha ya kuipongeza Wizara ya Malisili na Utalii kwa kusogeza hudama zake Kwa Jamii kupitia maonesho hayo Makubwa ya Kimataifa, ametoa wito Kwa watu Mbalimbali Kutumia fursa ya maonesho hayo yanayoendelea Jijini Dar es Salaam kujifunza, kuburudika na kuangalia fursa mbalimbali za kibahashara Kwa maendeleo binafsi na Taifa kwa ujumla.
Maonesho hayo ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam maarufu kama SabaSaba, ambapo Wizara ya Maliasili na Utalii ilikiwa sehemu ya washiriki, yameanza 28 Juni 2023 hadi 13 Julai 2023, huku yakiwa na kaulimbiu “Tanzania Mahali sahihi Pa biashara na Uwekezaji