Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifurahia jambo mara baada ya kukabidhiwa maua ya ukaribisho wakati alipowasili katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la kufanya kikao kazi cha kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa taasisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (hawapo pichani) jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Sehemu ya watumishi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na watendaji hao kilicholenga kuhimiza uwajibikaji.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Hassan Kitenge (Aliyesimama) akielezea utekelezaji wa majukumu ya taasisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene (Meza kuu katikati) wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti ya Ajira kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Katikati) na Naibu Waziri wake Mhe. Ridhiwani Kikwete (Wa kwanza kulia) wakimsikiliza Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Hassan Kitenge (Hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ofisi ya wakati wa kikao kazi cha Waziri huyo na Menejimenti ya Sekretarieti hiyo kilichofanyika jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bi. Leila Mavika.