Mfalme Zumaridi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuelekea kwenye sherehe ya kumshukuru Mungu baada ya kutoka Gerezani.
Mfalme Zumaridi akizungumza na waandishi wa habari juu ya sherehe ya shukrani aliyoandaliwa na Wafuasi wake itakayofanyika Julai 8 mwaka huu
……..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wafuasi wa Mhubiri Diana Bundala maarufu Mfalume Zumaridi wamemuandalia sherehe ya kumshukuru Mungu baada ya kutoka gerezani ambapo alikaa kwa muda wa mwaka mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari Jana Ijumanne Juni 27,2023 Mfalme Zumaridi alisema kuwa Wafuasi wake wameandaa sherehe hiyo kutokana na nguvu ya Mungu ilivyotumika kupitia kwa watu wakanisaidia kunitoa gerezani.
Amesema sherehe hiyo itafanyika Julai 8, 2023 nyumbani kwake mtaa wa Bugugu uliopo katika Kata ya Mkolani Wilayani Nyamagana ambapo itahudhuriwa na watu 2000.
” Nimekaa kwa muda mrefu sana bila kuongea na waandishi wa habari lakini leo hii nimewaita waandishi wa habari kwaajili ya kuzungumza na nyie kuelekea kwenye sherehe hii kubwa ya shukrani kwa Mungu wangu aliyenisimamia na kunivusha kwenye magumu mengi niliyopitia gerezani”, Alisema Mfalme Zumaridi
Alisema katika sherehe hiyo ya kihistoria itakuwa imeambatana na keki iliyobeba ujumbe wa maisha yake.
Mwisho Mfalume Zumaridi alitumia fursa hiyo kuwaombea waandishi wa habari ili wazidi kufanya kazi zao kwa weledi sanjari na kuliombea Taifa kwa ujumla liendelee kuilinda na kuitunza tunu ya amani iliyowekwa na Mungu.