Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bw. Adonis Bitegeko akifungua kikao kazi cha wadau wa mamlaka hiyo kilichofanyikakwenye ofisi za TMDA Mabibo jijini Dar es Salaam.
………………………………………..
NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM.
Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) leo tarehe 27/6/2023 Jijini Dar es Salaam wamekutana na
wadau wa wasambazaji wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa mfumo wa vifaa tiba na vitendanishi, kuwasikiliza pamoja na kupokea mawazo yao katika utekelezaji wa majukumu.
Akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha wadau cha kufanya tathimini na wasambazaji wa Dawa na Vifaa tiba kilichofanyika Ofisi za TMDA Mabibo jijini Dar es salaam, Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bw. Adonis Bitegeko, amesema kuwa kikao cha wadau kinafanyika kila mwaka na kushiriki wadau mbalimbali.
Bw. Bitegeko amesema kuwa wadau walioshiriki ni pamoja na sekta ya afya, wataalam wa ushauri wa vifaa tiba na vitendanishi, wasambazaji na wazalishaji.
“Kupitia mkutano huu ambao tunafanya kila mwaka pia tunatoa taarifa ya
maboresha ya kanuni na taratibu katika utekelezaji wa majukumu yetu” amesema Bw. Bitegeko.
Amesema kuwa wadau watapata fursa ya kuangalia taratibu zilizopo kwa ajili ya vifaa tiba na bidhaa kama zinazingatia ubora na ufanisi.
“Tunawapa mrejesho namna tunavyofatilia usalama kuhusu vifaa tiba na vitendanishi pamoja na kuwajengea uwezo na uwelewa zaidi” amesema
Bw. Bitegeko
Naye Mwenyekiti wa Chama cha waagiaji wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi (TAPI) Bw. Churchill Katwaza amesema mkutano huo unawasaidia sana kama wasambazaji kujua mambo muhimu ya kufanya kabla ya kuagiza vifaa Tiba na vitendanishi ili kuondoa changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwa waagiaji ambao baadhi hawajui kanuni na taratibu za uagizaji, hivyo hiyo ni kikao muhimu sana kwao ili kupata uelewa na kujiweka sawa kabla ya kuanza kufanya kufanya kazi hiyo.
Ameongeza kwamba kutofautiana kwa baadhi ya herufi za majina ya vifaa tiba hasa kwa nchi ambazo haziongei kiingereza kama China kifaa kinapokuja hapa na kubainika kuna herufi zinatofautiana huku mwagizaji alisajili kwa jina fulani.
Hii ni moja ya changamoto zinazotatiza shughuli ya uagizaji vifaa tiba ambapo inabidi muagizaji wasiliane na mamlaka zinazohusika ili kutatua changamoto hiyo jambo ambalo linafanya kuongezeka kwa gharama katika mnyororo mzima wa uagizaji kutokana na.
Katwaza ameongeza kuwa jambo lingine ni mamlaka nyingi kufanya kazi za aina moja mfano kifaa kimekaguliwa na TMDA lakini TBS na wao watataka lazima wakikague kifaa hichohicho, wakati mwingine na mamlaka nyingine zaidi hivyo kama serikali itaamua mamlaka zote ziwe katika eneo moja zinaweza kufanya kazi kwa pamoja kwenye eneo moja na kazi ikaenda kwa uharaka zaidi.
Rehema Mariki Meneja wa Usajili wa Vifaa Tiba na Vitendanishi akiwasilisha mada katika kikaokazi hicho kilichofanyika katika ofisi za TMDA Mabibo jijini Dar es Salaam.
Roberta Feruzi Afisa Mawasiliano Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA akitoa maelezo kadhaa wakati wa kikao kazi hicho.
Meneja wa Kanda ya Mashariki, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bw. Adonis Bitegeko akiwa katika kikao kazi cha wadau wa mamlaka hiyo kilichofanyikakwenye ofisi za TMDA Mabibo jijini Dar es Salaam. kulia ni Rehema Mariki Meneja wa Usajili wa Vifaa Tiba na Vitendanishi TMDA.
Rehema Mariki Meneja wa Usajili wa Vifaa Tiba na Vitendanishi TMDA akiwasilisha mada kwa wadau katika kikao kazi hicho.
Bi Rose Maingu Afisa Usajili wa Dawa Mamlaka ya Dawa na Fifaa Tiba TMDA akiwasilisha mada kwa wadau katikakikao kazi hicho.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mada katika kikao kazi hicho.
Picha ya pamoja.