Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akitoa Ufafanuzi kuhusu wanafunzi wanaoendelea na masomo nchini Kutoka nchi zilizoathiriwa na machafuko ya kivita.
Baadhi ya wanafunzi Kutoka nchini Sudan wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha MUHAS.
……………………..
Ameyasema hayo leo, tarehe 23 Juni 2023, wakati akichangia Bajeti kuu ya Serikali, akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Janejelly James Ntate, kuhusu wanafunzi wanaorejea nchini kutokana na vita na machafuko yanayoendelea katika nchi mbili, Ukraine na Urusi, na ghasia nchini Sudan, katika Ukumbi wa Bunge, Jijini Dodoma.
“Nichangie kuhusu wanafunzi wanaotoka Ukraine kutokana na vita kati ya Ukraine na Urusi, na wale wanaotoka Sudan kutokana na ghasia zinazoendelea katika nchi hizo. Kwanza kabisa, niweke wazi kuwa nchi yetu inaendelea kuwa na amani kutokana na jinsi tunavyoendesha siasa zetu kwa utulivu, heshima, na kwa kumuunga mkono kiongozi wetu,” alisema Profesa Mkenda.
“Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Ukraine wameomba kuhamia vyuo vya Tanzania, na taratibu za uhamisho wa masomo, unaoitwa ‘credit transfer’, zimefanyika na baadhi yao wamejiunga na vyuo vyetu. Uhamisho wa vyuo vikuu kutoka nje na kujiunga na vyuo vya ndani unasimamiwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), na vigezo vingi vinazingatiwa. Aidha, kwa wanafunzi waliotoka Sudan, hakuna hata mmoja ambaye amejiunga na vyuo vyetu. Vikao vitakavyoangalia uwezekano wa uhamisho wao vitafanyika kesho,” alisema.
Profesa Mkenda aliongeza kuwa kuna changamoto katika kuafikiana kwa vigezo vinavyotumiwa katika kuchagua wanafunzi wanaopokelewa katika vyuo vya nje, na suala hilo linasimamiwa na TCU kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu na Amali ya Zanzibar ili kupata njia bora ya kuwadahili wanafunzi hao katika vyuo vyetu vya ndani. “Hili ni jambo tunalolipa umuhimu na tunafanya kazi kwa karibu na TCU na Wizara ya Elimu na Amali ya Zanzibar ili kupata suluhisho la changamoto hiyo,” alisisitiza Profesa Mkenda.
Prof. Mkenda alieleza kuwa wanafunzi wote wamepokelewa na Prof. Mohamed Janabi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ( MNH), sio Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha MUHAS inayoongozwa na Profesa Andrea B. Pembe. Wanafunzi hao kutoka Sudan walionekana katika picha na wamekwisha soma kwa miaka mitano, na sasa watashiriki majaribio ya kliniki hapa Tanzania. Baada ya kumaliza, watare