Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akieleza jambo kuhusu Mswada wa Sheria ya Fedha ulipowasilishwa bungeni jijini Dodoma, kulia ni Naibu wake, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb)
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu wake, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakipongezwa na baadhi ya wabunge baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2023/2024 kwa asilimia 95.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Lawrance Mafuru, katika viwanja vya Bunge, baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2023/2024 kwa asilimia 95.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiwa katika picha na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El- maamry Mwamba, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2023/2024 kwa asilimia 95.
Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo, akifafanua jambo bungeni wakati wa mjadala wa Mswada wa Sheria ya Fedhawa Mwaka 2023/2024, ambao umepitishwa na Bunge.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu wake, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakipongezana katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2023/2024 kwa asilimia 95.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu wake, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El- maamry Mwamba (wa sita kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Manaibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Lawarance Mafuru (wa nne kulia), Bi. Amina Khamis Shaaban (wa tano kushoto), wakuu wa Idara na Vitengo na wadau wengine nje ya ukumbi wa Bunge, baada ya Bunge kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2023/2024 kwa asilimia 95.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)