Serikali kupitia Wizara ya Kilimo, imebadilisha kanuni zake kuanzia msimu ujao wa kilimo vifungashio vya mbolea vitakuwa katika ujazo wa kuanzia kilo moja na kuendelea.
Hapo zamani ujazo wa mbolea za kilimo ilikuwa ni kuanzia kilo 25 na kuendelea.
Hii imetokana na kilio cha wananchi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, katika ziara yake Mkoani Dodoma kuomba chama kiingilie kati ili wananchi wamudu bei ya mboleo yenye ujazo wa kuanzia kilo moja na kuendelea.
Kutokana na hali hiyo Katibu Mkuu wa CCM amemtaka Waziri wa Kilimo kutoa kauli katika suala hilo.
Katika mkutano wa hadhara wa hitimisho ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Chongolo, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ametangaza utaratibu huo mpya wa ujazo wa mbolea kuanzia kilo moja msimu ujao wa Kilimo.