Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mhe. Mohamed Msofe akizungumza na wanachama wa Kata ya Kitunda akiwa katika ziara na kamati ya Utekelezaji Wazazi (W) Ilala.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mhe. Mohamed Msofe (kulia) akimkabidhi kadi na kitini Cha mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa Matawi Kata ya Kitunda.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Bw. Mtiti Jirabi akitoa maelekezo katika Kikao kazi na wanachama wa Jumuiya hiyo Kata ya Kitunda.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Bw. Edward Haule akizungumza na Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kitunda.
Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala, pia Diwani wa Kata ya Kariakoo, Bw. Abdulkarim Masamaki akizungumza na Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Kitunda.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Bw. Shamsudin Ahmed akizungumza na Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Kitunda.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala, Mwanaisha Mrutu akizungumza na Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Kitunda.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Kitunda Bw. Frank Kanyenye akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM katika Kata hiyo.
Diwani wa Kata ya Kitunda Victor Uedasto akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM katika Kata hiyo.
Baadhi ya Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kitunda wakitoa kero na mapendekezo kwa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Ilala.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mhe. Mohamed Msofe ametoa wito kwa Wanachama wa Jumuiya hiyo Kata ya Kitunda kutengeneza mifumo ya kujiingizia fedha kwa kubuni miradi yao wenyewe, huku akibainisha kwa kushirikiana na kamati ya utekelezaji wapo tayari kuwasaidia.
Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati ya Utekelezaji Wazazi CCM (W) Ilala tarehe 23/6/2023 kufanya ziara Kata ya Kitunda na kuzungumza na wanachama wake kwa ajili ya kuangalia uhai wa Jumuiya katika matawi na mashina na kubaini baadhi ya changamoto ikiwemo mikopo ya kausha damu ambayo inawatesa baadhi ya wanachama na kushindwa kushiriki kikamilifu kazi za Jumuiya.
Akizungumza na wanachama wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Kitunda, Mwenyekiti Mhe. Msofe ametumia fursa hiyo kuipongeza tawi la Kitunda kati kwa kuanzisha kikoba na kukopeshana wao wenyewe bila kutumia mikopo ya kausha damu.
“Tuige mfano wa Tawi la Kitunda kati utawasaidia, pia anzisheni miradi kwa kukopeshana bidhaa” amesema Mhe. Msofe.
Amesema kuwa mikopo ya kausha damu inazalilisha familia kwani kuna siku biashara yako inaweza kutopata wateja na wao kila siku wanataka fedha yao kwa ajili ya marejesho.
Ameeleza kuwa wanagawa kadi 50 za wanachama wa jumuiya ya wazazi kwa kila tawi bure kama mtaji kwao kwani watakwenda kuuza kwake wanachama.
“Mkiuza leteni ripoti kwa Katibu Kata ili awape kadi nyengine baada ya miezi mitatu tutarudi tena, nendeni mkatoa kadi kuongeza wanachama” amesema Mhe. Msofe.
Katibu wa Elimu, Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala, pia Diwani wa Kata ya Kariakoo, Bw. Abdulkarim Masamaki, amesisitiza umuhimu wa viongozi kufanya kazi kwa umoja ili kuleta maendeleo ya Jumuiya yenye tija.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Bw. Edward Haule, amesema kuwa katika ziara hiyo wamebeba ajenda ya uchumi wa Jumuiya ya Wazazi kwa kila Kata.
Bw. Haule amesema kuwa ili kufika katika uchumi mzuri Jumuiya ya wazazi inapaswa kuwa na ushirikiano kuanzia ngazi ya tawi na shina, kwani lengo lao ni kuhakikisha wanachama wanakuwa na faraja, amani na kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
“Heshima ya mtu ni kitu, heshima ya Jumuiya hii tutafuteni uchumi, tukiwa na uchumi yote yanawezekana, nasema hivi kwa sababu nina upendo na nyinyi” amesema Bw. Haule.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala Bw. Shamsudin Ahmed, amewataka
viongozi wa Kata ya Kitunda kuongeza juhudi katika utendaji kazi ili kuongeza idadi ya wanachama katika Jumuiya ya Wazazi.
“Bado muda tunao wa kufanya maandalizi ili kuendelea kuongeza idadi wanachama pamoja na kufatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yetu” Bw. Ahmed.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Ilala, Mwanaisha Mrutu, amesema kuwa wakati umefika wa kufanya maamuzi ya utekelezaji katika nyanja mbalimbali ili kuleta tija kwa Jumuiya.
Kamati ya Utekelezaji Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala itaendelea na ziara katika Kata ya Gongo la Mboto na Ukonga tarehe 25/6/2023.