Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amekema tabia ya udokozi na wizi unaofanywa katika miradi mbalimbali hali inayopelekea kukwamisha maendeleo katika maeneo husika.
Aidha amesema wizi unaofanywa na baadhi ya watu katika miradi hiyo ni makosa ya uhujumu uchumi na unasababisha hasara kwa Serikali kwa kuwa inatumia gharama kubwa kufidia wizi huo.
Chongolo amekemea hayo alipotembelea mradi wa barabara ya mzunguko inayojengwa katika eneo la Veyula Wilaya ya Dodoma Mjini ikiwa ni sehemu ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi katika Wilaya hiyo.
Akizungumzia mradi huo amesema unaenda kufungua jiji la dodoma na kutoa taswira ya kiuchumi kutokana ma ukubwa wake.
Mradi huo ni wa Km 112 na unagharimu Bilioni 220 ambapo ukikamilika utakuwa ni moja ya barabara ndefu zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo itazunguka jiji la Dodoma.