Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela akifungua maonyesho hayo jijini Arusha
Wadau mbalimbali waliohudhuria  katika maonyesho hayo jijini Arusha yanayofanyika  katika viwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Julieth Laizer, Arusha 
 
 

“Niwaase vijana kutumia fursa hii katika kupata elimu na kuweza kujiepusha na utumiaji wa madawa ya kulevya, kwani athari za utumiaji madawa ya kulevya ni kubwa maana inapelekea vitendo vya uvunjifu wa amani”. amesema Mongela.

“Kipindi cha uongozi huu wa awamu ya  6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejitahidi kuongeza vituo vya kutoa tiba kwa warahibu na kuweza kuwarudisha katika sehemu ya jamii yetu na hata kuwa wajasiriamali na kuendelea kuwa tegemeo kwa familia zao”. ameongeza Mongela

Aidha   Mongela ameiomba jamii wakati Taifa linaendelea na maadhimisho haya ya kupinga na kupambana na madawa ya kulevya jmiendelee kuwasaidia waathirika wa madawa hayo na kuacha kuwanyanyapaa maana siyo watu wa kuwatenga kwa namna moja ama nyingine.

“Tumeona mamlaka husika imepambana kufanya oparesheni ( Msako maalum ) katika kupambana ipasavyo na madawa haya hasa bangi kwa wale wanao lima zao hilo sambamba na kutoa elimu kwa jamii”.amesema Mongela.

Aidha ametoa  rai kwa watanzania wenzangu waendelee kujua bado sheria zetu ziko pale pale wasikengeuke na kujifanya wameziba macho na siyo kwamba hawata julikana kwa kufanya biashara hizo za kuuza madawa ya kulevya au kwa kujihusisha na kilimo cha bangi”. Ameongeza 

Aidha Mongela amewaomba wananchi wa Mkoa wa Arusha kuendelea kushirikiana na kuweza kumpokea Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Juni 25, 2023 katika kilele cha kupambana na dawa za kulevya na kuweza kuungana kwa pamoja katika kupinga vita madawa ya kulevya.

Hata hivyo Mongela amezindua kitabu maalumu cha kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya, kitabu kilicho andikwa na mdau wa kupinga na kupambana na madawa ya kulevya hapa nchini ambaye ameandika kitabu hicho kwa lengo la kuokoa jamii.