Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongela akifungua maonyesho hayo jijini Arusha
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika maonyesho hayo jijini Arusha yanayofanyika katika viwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Julieth Laizer, Arusha
“Kipindi cha uongozi huu wa awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejitahidi kuongeza vituo vya kutoa tiba kwa warahibu na kuweza kuwarudisha katika sehemu ya jamii yetu na hata kuwa wajasiriamali na kuendelea kuwa tegemeo kwa familia zao”. ameongeza Mongela
“Tumeona mamlaka husika imepambana kufanya oparesheni ( Msako maalum ) katika kupambana ipasavyo na madawa haya hasa bangi kwa wale wanao lima zao hilo sambamba na kutoa elimu kwa jamii”.amesema Mongela.
Aidha ametoa rai kwa watanzania wenzangu waendelee kujua bado sheria zetu ziko pale pale wasikengeuke na kujifanya wameziba macho na siyo kwamba hawata julikana kwa kufanya biashara hizo za kuuza madawa ya kulevya au kwa kujihusisha na kilimo cha bangi”. Ameongeza