Picha mbalimbali za Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza katika kikao cha nje kilichofanyika katika uwanja wa CCM Chali Sanga, wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
Kikao hicho ambacho kimehitimisha ziara ya Katibu Mkuu katika wilaya ya Bahi ambapo pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu aliweza sikiliza wananchi, kutembelea miradi ya maji Ibihwa, skimu za umwagiliaji, hospitali ya Wilaya ya Bahi na mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi.
Katika ziara hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025 pamoja na kuimarisha uhai wa Chama, Katibu Mkuu aliongozana na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu.