Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti inawaalika wadau kutoa maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2023 kwa mujibu wa Kanuni ya 97(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti inawaalika wadau kutoa maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2023 kwa mujibu wa Kanuni ya 97(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023.
Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) utafanyika siku ya Alhamisi na Ijumaa tarehe 22 na 23 Juni, 2023 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.
Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Muswada huo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.
Vilevile Kamati itapokea maoni kwa njia ya posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo:- Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge, 10 Barabara ya Morogoro S.L.P. 941, 40490 Tambukareli, DODOMA.
Barua pepe: [email protected] na [email protected] huo pia unaweza kupakuliwa katika tovuti ya Bunge, www.bunge.go.tz.
Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua pepe tajwa endapo utapenda kuwasilisha maoni yako kwa kuzungumza kwa ajili ya hatua za kiutawala.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge,S.L.P 941, DODOMA. 20 Juni, 2023..
Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) utafanyika siku ya Alhamisi na Ijumaa tarehe 22 na 23 Juni, 2023 saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.
Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Muswada huo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.
Vilevile Kamati itapokea maoni kwa njia ya posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo:- Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge, 10 Barabara ya Morogoro S.L.P. 941, 40490 Tambukareli, DODOMA.
Barua pepe: [email protected] na [email protected] huo pia unaweza kupakuliwa katika tovuti ya Bunge, www.bunge.go.tz.
Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua pepe tajwa endapo utapenda kuwasilisha maoni yako kwa kuzungumza kwa ajili ya hatua za kiutawala.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,S.L.P 941, DODOMA. 20 Juni, 2023.