Raisa Said,Tanga
Wazazi, walezi na jamii kwa ujumla imetakiwa kusimamia majukumu yao
ipasavyo kwa watoto kuanzia mwaka sifuri hadi miaka name lengo ni kuwalinda na athari mbalimbali ikiwemo ukatili pamoja na matumizi mabaya ya
mitandao ya kijamii.
Wito huto umetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya
alipokuwa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika Jijini Tanga.
.
Katika maadhimisho hayo halmashauri ya jiji la Tanga imetoa msaada wa
vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwenye vituo vya kulelea watoto
wanaoishi kwenye mazingira magumu ambapo katika kituo cha Nyumba ya
furaha imetoa kilo 20 za mchele, kilo 40 za Maharage na vyandarua 10
wakivipatia vituo 6 vilivyopo hii ikiwa ni njia ya kuonyesha kuwajali
na kuwathamini watoto hao
Mikaya amesema kutokana na mabadiliko ya kidigital Dunia
imebadilika sambamba na matukio mengi ya kiukatili dhidi ya watoto
yakishamiri hivyo wazazi, walezi na jamii kwa ujumla wana jukumu kubwa
la kuhakikisha wanakiandaa kizazi ambacho kitakuwa ni tegemeo la
kesho.
“Wazazi walezi tunapaswa kujua kwamba mtoto naye ana haki yake,
ikiwemo kusikilizwa, kulindwa na kuangaliwa kwa umakini niwaombe sana
wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia usalama wa mtoto kuanzia mwaka 0-8 ili tuwe na Taifa lenye vijana waadilifu baadaye ambao
watalisongeza taifa letu mbele katika mbalimbali za kiuchumi” Alieleza Katibu Tawala huyo
Amesema kuwa kuna mambo mengi ambayo sasa hivi yanaendelea katika
jamii. Alieleza kuwa dunia imebadilika na ipo kwenye mfumo wa
kidigital ambapo kuna mambo mengi yanafanyika wakati huu ikiwemo
ukatili kwa watoto ,unyanyasaji , ubakaji, matumizi mabaya ya mitandao
kuna Uhuru mkubwa sana upo kwa watoto, amesema Mikaya.
Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wa jiji la Tanga Simon Mdende
amesema bado hali ya unyanyasaji kwa watoto hususan kuanzia miaka
sifuri hadi miaka nane katika jamii si shwari licha ya elimu
inayoendelea kutolea katika jamii kwa maslahi ya mtoto huku. Mdende
aliwataka wahisani mbalimbali kujitokeza kuvisaidia vituo vinavyolea
watoto ili waweze kupata malezi na huduma bora wanazostahili.
Alieleza kuwa katika halmashauri ya jiji la Tanga kwa watoto wanaoishi
kwenye halmashauri ya jiji la Tanga hali si nzuri sana kwa sababu
watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wamechukuliwa kutoka sehemu
tofauti na wengi wanapowatoa kwenye mazingira waliyozoea wanaathirika
kisaikolojia. “Katika hivi vituo wanapoishi hawa watoto bado uchumi
sio mzuri sana kwa hiyo jamii inahitajika sana kujitoa na kusaidia
hawa watoto ili kupata huduma mbalimbali” alisema Mdende.
Kwa upande wake Afisa ustawi wa jiji la Tanga Deogratias Casmiri
amewataka wazazi na walezi pamoja na majukumu mengine kukaa karibu na
watoto kubaini changamoto zinazowakabili katika mazingira ya nyumbani
na mashuleni na hatimaye kuzitatua mapema kabla hawajaathirika kwa
namna yeyote ile ili kuwa na kizazi bora Cha baadaye.
“Tusipoweka nguvu ya kutosha katika malezi ya watoto
ustawi wa watoto hatuupati, ustawi wa mtoto maana yake apate huduma
zote za msingi ikiwemo chakula, malazi, elimu muda wa kukaa karibu na
wazazi, walezi wake , Usimamizi wa haki za mtoto unaanzia kwa mazazi
mlezi na jamii yote kwa ujumla kwa mujibu wa Sheria za nchi yetu
jukumu la kuwaangalia watoto ni la kila raia” alisema Casmiri.
Wakizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo mkurugenzi wa kituo
cha Goodwill and foundation Sayid Muhzari Aidarus na mlezi wa kituo
cha Nyumba ya Furaha Sister Sarah Francis wameeleza hisia zao juu
ya msaada hi uliotolewa na halmashauri wakiwataka wadau na wahisani
mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia watoto waliopo katika vituo
hivyo hii Ni kutokana na mahitaji yao huku vituo vikielemewa kutokana
na uchumi mdogo.
“Kwa niaba ya taasisi niwapongeze na niwashukuru sana kwaajili ya
tukio hili adhimu na lenye thamani juu ya mtoto, watoto Hawa Wana
ufahamu na pale wanapoona jamii haiitikii kuja kwao wanahisi kwamba
wametengwa kwahiyo tusipokuja Kama hivi Tutajenga Taifa la watu wenye
roho mbaya na roho ngumu kwa sababu wataona hawapotezi chochote
kwahiyo kuja kqenu mmewakilisha mamilioni ya watanzania” alisema
Aidarus.
“Kwa niaba ya masister na watoto wa kituo cha Nyumba ya Furaha
tunashukuru sana kwa yale yote ambayo mmetutendea Kama serikali
katika kituo chetu na vituo vyote ambavyo mnatoa misaada hii Hawa
watoto tuliokuwepo nao Wana mahitaji ya vitu vingi na hqki zao za
msingi zinatakiwa zitolewe Kama watoto wengine waliolelewa na wazazi
wawili” alisema Sister Sarah.
Siku ya mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa kila mwaka kwa mwaka huu kauli mbiu ni “Zingatia usalama wa mtoto katika ulimwengu wa kidigital.