Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo amewataka wazazi na walezi Nchini kuongeza juhudi katika malezi kutokana na kukithiri kwa mmomonyoko wa maadili kwa watoto kwa sasa.
Akizungumza leo 20.6.2023 na wananchi wa kata ya Mondo katika ziara yake katika Wilaya ya Chemba, Chongolo amesema watoto wengi wanatia aibu kwa sasa kutokana na kuharibika kimaadili.
Amesema mmomonyoka wa maadili kwa watoto kwa kiasi kikubwa umesababishwa na malezi ya wazazi ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo na hivyo watoto kuharibika.
Katibu Mkuu amesema yakitengenezwa mazingira mazuri ya kuwalea watoto katika maadili kutasaidia kujenga misingi sahihi kwa watoto na hata kwa Taifa.
Katibu Mkuu Daniel Chongolo bado yupo katika Mkoa wa Dodoma akikagua Uhai wa Chama na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ambapo ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi na Katibu wa NEC-Oganaizesheni.