Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu
Na Eleuteri Mangi, WUSM, Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na kufanya kikao na vijana waanzilishi wa UNI AWARDS na kujadili namna bora ya kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana wanaosoma vyuo mbalimbali nchini.
Kikao hicho kimefanyika Juni 20, 2023 jijini Dar es salaam ambapo wamejadili maandalizi ya kuandaa tamasha la ni kuinua na kuendeleza vipaji kwa wanafunzi wanasoma vyuo nchini.
Bw. Yakubu amewapongeza vijana hao wakiongozwa na Bw. Joseph Ndaro ambaye ni mwasisi wa jukwaa hilo na kuwahimiza kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa ushirikiano ili waendelee kuwa chanzo kikubwa cha kuwaajiri vijana kupitia vipaji vyao na kujitengenezea fursa za ujasirimali kipindi wakiwa vyuoni na baada ya kuhitimu.
Akizunghumzia jukwaa hilo, Bw. Ndaro amesema tamasha la mwaka 2023 ni la tano kufanyika ambapo tamasha la kwanza lilifanyika mwaka 2019 kwa vyuo vilivyopo Dar-es-salaam pekee na miaka inayofuta ya 2020 hadi 2022 limefanyika kwa vyuo vyote Tanzania na kufanikiwa kuzunguka mikoa nane ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Dar es salaam.