Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Angelina Ngalula akizungumza leo tarehe 19/6/2023 katika mjadala ambao umeandaliwa Kampuni ya Media Brains uliokuwa na majadiliano yaliyojikita katika Mkataba wa Kiserikali (IGA) uliohusisha serikali ya Dubai na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhusu maendeleo ya bandari.
Baadhi ya washiriki wakati wa mjadala wa kitaifa uliolenga kulinda na kuendeleza umoja wa kitaifa wakati wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Wadau wa Maendeleo wakiwemo viongozi wa dini wameitaka Serikali kutoa ufafanuzi na kuelimisha jamii kuhusu mkataba wa Bandari ya Dar es Salaam jambo ambao litaleta tija kwa maslahi mapana ya Taifa la Tanzania.
Wakizungumza leo tarehe 19/6/2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mjadala wa kitaifa uliolenga kulinda na kuendeleza umoja wa kitaifa wakati wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Angelina Ngalula, amesema kuwa sekta binafsi ni engine ya uchumi kwa sababu kupitia shughuli zake h
utengeneza ajira zaidi ya asilimia 80 kwenye nchi zinazoendelea.
Ngalula amesema kuwa sekta binafsi wanatakiwa kuwa na moja katika mjadala wa bandari katika kujikita kuzungumzia agenda iliyopo badala ya kumshambulia mtu.
“Tumezikosa fursa nyingi kwa muda mrefu ambazo zingeweza kubadilisha uchumi wa nchi kwa sababu sisi tumekaa kama kisiwa katika mufanya shughuli ya bandari, lazima kusimamia mnyororo mzima wa usafirishaji” amesema Ngalula.
Amesema kuwa Bandari ya Dar es Salaam inafanya kazi kwa njia ambayo inahitaji uwekezaji mkubwa katika teknolojia mpya za utunzaji na uhifadhi wa mizigo.
Mfanyabiashara Rostam Aziz, amesema kuwa amesikitishwa na aina ya majadiliano kuhusu bandari ya Dar es Salaam ambayo imejikita katika misingi ya udini, siasa na ukabila ambapo ni hatari kwa usalama wa nchi.
Amesema kuwa mjadala wa Bandari ya Dar es Salaam ni mjadala wa uchumi, lakini kuna sauti zinazoibuka ambazo zinaleta migawanyiko kwa kuingiza ajenda za siasa.
Mfanyabiashara huyo amesema kuwa mjadala huo unaendeshwa kishabiki, hivyo sekta binafsi zinapaswa kuendesha bandari hiyo kwani ni jambo la busara.
Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Charles Kitima, amesema kuwa katika mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi Tanzania yanahitaji kuelimishana.
Kitima amesema suala la uchumi wa nchi ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa kwani Hayati Mwalimu Nyerere aliamini katika ushirikiano na sekta binafsi nchini.
“Tunapaswa kusikiliza sauti ya wawekezaji wa ndani ili kuangalia namna ya kuboresha maendeleo ya Taifa” amesema Kitima.
Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amesema ipo haja ya kuunda kampuni ya uendeshaji ya Bandari ya Dar es Salaam ambayo itaingia ubia na DP World kufanya kazi kwa pamoja.
Kabwe amesema kuwa uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam inaitaji ushirikiano ili kuwezesha ushirikishwaji wa wenyeji jambo ambolo litakuwa na tija kwa Taifa.
“Uwepo wa kampuni hiyo itasaidia kuendeshwa kwa ufanisi, na inaweza kumilikiwa na wageni au wazawa ili wapate uwezo wa kuendesha bandari” amesema Kabwe.
Mwakilishi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Godbless Lema, amesema hakuna udini katika masuala ya uwekezaji wa bandari baadhi wanajaribu kuzuia hoja kwa kuweka masuala ya dini kwenye mjadala huo.
Mfanyabiashara huyu amesema kuwa Taifa la Tanzania linaitaji mwekezaji zaidi ya bandarini ili kuleta ufanisi na kukuza uchumi.
Mdahalo huo umeandaliwa na Kampuni ya Media Brains uliokuwa na majadiliano yaliyojikita katika Mkataba wa Kiserikali (IGA) uliohusisha serikali ya Dubai na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhusu maendeleo ya bandari.